Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akifanyamahojino na
Mtangazaji wa Redio Time FM ya Jijini Dar es Salaam hivi karibuni
Na: Grace Semfuko,MAELEZO
Serikali imeongeza bajeti ya
Vifaa tiba kutoka shilingi Bilioni 31 hadi kufikia Bilioni 270 katika kipindi
cha Miaka mitatu na kujenga Vituo vya afya zaidi ya 352 pamoja na hospitali
kubwa 67.
Hayo yamebainishwa na
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hssan Abbasi takati wa mahojiano na kipindi cha
Mseto on Saturday kinachorushwa na kituo cha Redio Times cha Jijini Dar Es
Salaam.
Dkt Abbasi alisema hatua
hiyo ya kuongeza bajeti ya afya ni kuimarisha uhakika wa huduma hiyo kote
nchini na kuwataka watanzania kunufaika na huduma hizo.
Alisema hivi sasa Serikali
imeondokana na tabia ya ununuzi wa dawa kutoka kwa madalali wa kawaida na sasa
inanunua dawa hizo kutoka viwandani hali ambayo imeipa unafuu wa kuwa na dawa
na vita tiba vya uhakika.
“ Yaani mtu yupo tu huko
Kariakoo, hana kiwanda wala duka la dawa, anapewa tenda ya dawa, na yeye
akishapewa hiyo tenda aagize tena dawa huk zinakotoka, hou ujanja unjanja sasa
haupo tena, sasa tunaagiza dawa wenyewe toka viwandani na sio kuwatumia madalali
wa kati hapa,ndio maana mnaona hakuna tena changamoto za dawa huko hospitalen”
alisema Dkt Abbasi.
Akizungumzia suala la ajira
Dkt Abbasi alisema zaidi ya wafanyakazi 8,000 wa Sekta ya afya wakiwepo
Madaktari, wafamasia na wahudumu mbalimbali wameajiriwa na wapo vituoni
wanafanya kazi.
Aidha alisema Serikali
imeanza kuleta vifaa tiba vya kibingwa nchini vitakavyotumiwa kwenye kwenye
hospitali kubwa nchini na kuifanya nchi
kuwa katika viwango vya hali ya juu kabisa vya matibabu ukilinganisha na nchi
nyingine za Afrika Mashariki.
“ Sasa Tanzania imekuwa ni
nchi ya ufadhili wa matibabu kwa baadhi ya chi za Afrika au kwa lugea ya kigeni
ni Donor Country, kwani inatoa tiba kwa baadhi ya raia wa nchi nyingine, kuna
watu niliwaambia tutafika huko wakawa wanakataa, sasa hivi waseme lingine”
Katika kuzidi kuimarisha
Sekta ya afya nchini Tanzania imeanza kupandikiza figo ambapo wagonjwa
waliokuwa wakienda nje kutibiwa hivi sasa huduma hizo zinapatikana nchini kwa
gharama nafuu ukilinganisha na chi nyingine.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni