Jumatatu, 24 Juni 2019

Serikali Awamu ya Tano ni Inaongozwa Kisayansi - Dkt. Abbasi




Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akifanyamahojino na
Mtangazaji wa Redio One ya Jijini Dar es Salaam hivi karibuni


Na: Antony Benedicto, MAELEZO
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi amesema Serikali imeendelea kutekeleza bajeti yake katika ujenzi wa miradi mbalimbali kwenye sekta zote ambapo ujenzi wa Reli ya kisasa ya Standard Gauge (SGR) tayari zaidi ya asilimia 50 za awamu ya kwanza ya ujenzi huh kutoka Dar Es Salaam hadi Morogoro zimeshajengwa.

Dkt Abbasi pia alisema hivi sasa Serikali imejenga zaidi ya Hospitali kubwa 67 patika kipindi cha miaka mitatu tu ya utekelezaji wa Bajeti ukilinganisha na zile 77 zilizojengwa kabla na wakati wa uhuru huku dawa na vifaa tiba vikipatikana kwenye hospitali zote nchini kwa asilimia 90.

Aliyasema hayo wakati wa mahojiano na Radio One Stereo katika kipindi cha Kumepambazuka ambapo alizungumzia utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/2020 na kusema kuwa hivi sasa changamoto za Kijamii kwa watanzania zimepungua kwa asilimia 80.

“Hii ni Serikali ya kisayansi, inatatua changamoto za kijamii kwa kasi zaidi ukilinganisha na huko nyuma, tupo vizuri naomba watanzania mtembee kifua mbele, Serikali yenu ipo kazını” alisema Dkt Abbasi.

Aidha katika mahojiano na kipindi hicho Pia Dkt Abbasi alitumia fursa hiyo kuwatoa hofu Watanzania kuhusiana na usalama wa nchi na kuwataka kupuuza taarifa za mitandaoni zinazojaribu kuichafua taswira ya Tanzania.

“Naomba niwatake Watanzania mpuuze taarifa za mitandaoni zinazojaribu kuichafua nchi yetu, kuna watu wachache wanaodhani Watanzania tumelala, ndugu zangu kuna watu katika nchi hii hawalali wanahakikisha tunakuwa salama kila siku, sasa kikundi tu cha watu kinaibuka na kusema eti sijui kuna shambulio hizo ni taarifa za uongo, zipuuzeni” alisema Dkt Abbasi.

Akizungumzia Suala la Elimu Dkt Abbasi alisema Serikali ya awamu ya tano imeweza kuboresha miundombinu ya elimu, kuajiri walimu na kujenga madarasa kwenye shule mbalimbali nchini na hive kuongeza tija ya ufaulu.

Alisema hive sasa Serikali imetenga shilingi Bilioni 23 kila mwezi kwa ajili ya kutoa elimu bure kwa wanafunzi nchini hali ambayo imeongeza uandikishaji wa wanafunzi mashuleni.

“Kama mnavyojua zamani watoto Wengi walikuwa hawaendi shule, kufuatia mkakati wa Serikali ya Magufuli wa kuimarisha elimu na kutoa fursa ya elimu bure nchini kumekuwa na ongezeko kubwa sana la Wanafunzi mashuleni, hili si jambo dogo” alisema Dkt Abbasi.


 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Kumbukumbu la Blogu