|
Mstahiki Meya wa Jiji
la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe, akieleza umuhimu wa kuzingatia mbinu za
ufanyaji wa tafiti zenye kuzingatia viwango vya kimataifa katika ,wakati
akifungua warsha ya watafiti kutoka nchi tano za Afrika, katika Chuo cha
Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
|
Watafiti nchini
wametakiwa kuweka mkazo katika mbinu za utafiti zinazokidhi viwango vya
kimataifa ili kuwa na majibu ya tafiti zenye tija zilizo na lengo la kutatua
changamoto katika jamii ya watanzania na duniani kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa na
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe, alipokuwa akifungua warsha
ya Watafiti kutoka nchi ya Kenya, Afrika Kusini, Rwanda, Uganda na wenyeji
Tanzania, uliofanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP)
jijini Dodoma.
Mtahiki Meya
Mwamfupe, alisema kuwa ili utafiti uwe na thamani nilazima kutumia mbinu
zinazoaminika bila kujali utafiti unaofanyika unahusu kitu gani, kwa lengo la
kuondoa mkanganyiko wa matokeo hivyo kuwa na tija kwa jamii.
|
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda,
akitoa mada katika warsha ya watafiti kutoka nchi tano za Afrika, katika Chuo
cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma, ambapo alieleza
mikakati ya Serikali kukuza uchumi na ajira nchini.
|
|
Watafiti kutoka nchi
ya Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Rwanda na wenyeji Tanzania, wakifuatilia mada
kuhusu changamoto za kiuchumi Afrika na mikakati ya kukabiliana nayo ikiwemo
kuwa na uchumi wa viwanda, iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na
Utalii Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani),
katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
“Utafiti wa kisayansi
ni ule unaotumia njia zinazokubalika kimataifa na kuwa na uwezo wa kukabiliana
na changamoto zikiwemo za kutokuwa na usawa hasa katika pande mbili za Dunia
yani Kasikazini na Kusini lakini pia katika jamii moja na nyingine”, alieleza
Meya Prof. Mwamfupe.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda,
ambaye alikua mtoa mada katika warsha hiyo alisema kuwa, katika wasilisho lake
wadau kutoka nje ya nchi wamefurahishwa na uchambuzi kuhusu hali ya uchumi
ambapo ilielezwa namna watu wenye kipato kikubwa kupenda kununua bidhaa nje
jambo ambalo limeifanya Serikali ya Tanzania kuweka mikakati ya kutatua tatizo
hilo ili kujenga uchumi wa bnchi.
|
|
Mhandisi wa Chuo
Kikuu cha Munich Ujerumani Prof. Walter Vries, akisikiliza kwa makini maelezo
ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda (kushoto), wakati wa warsha ya
watafiti kutoka nchi tano za Afrika, katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo
Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
|
|
Mstahiki Meya wa Jiji
la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na
wadau wa utafiti kutoka Ujerumani, Kenya, Uganda, Afrika Kusini na Rwanda,
wakati wa warsha ya watafiti wanaochipukia, katika Chuo cha Mipango ya
Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
|
|
Mstahiki Meya wa Jiji
la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na
wadau wa utafiti kutoka baadhi ya halmashauri nchini, na wengine kutoka nchi ya
Kenya, Uganda, Afrika Kusini na Rwanda wakati wa warsha ya watafiti
wanaochipukia, katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini
Dodoma.
(Picha na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
Alisema kuwa tabia ya
wenye kipato kikubwa kununua bidhaa nje kuna kosesha ajira, hivyo Serikali
imeamua kuweka mikakati ya Ujenzi wa uchumi katika Nyanja ya viwanda, kilimo na
miundombinu ikiwemo ya umeme, jambo ambalo ni ajenda ya Afrika
Kwa upande wake
Mratibu wa Warsha hiyo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Cha Mipango Vijijini,
Dkt. George Kanyasi, alisema kuwa lengo la Warsha hiyo ni kuwakutanisha
watafiti wanaochipukia na wanasayansi kutoka nchi tano za Afrika kwa lengo la
kuwajengea uwezo ili kupata watafiti mahiri.
Amesema kuwa kazi ya
tafiti sio tu kuongeza maarifa lakini pia kutatua changamoto katika maeneo
yaliyokosa usawa katika elimu, uchumi, siasa na masuala ya kijamii
Mkutano huo pamoja na
kuwashirikisha watafiti kutoka nje ya nchi, pia umewahusisha baadhi ya wadau
kutoka Halmashauri ili kujua changamoto zao na kuweka mikakati ya kuzitatua,
aidha warsha zinazofuata zitawakutanisha Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa
Mipango ili waweze kubaini matatizo ya maeneo yao na waweze kuyatatua.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni