Jumamosi, 11 Juni 2016

Wananchi wajitokeza kwa wingi maonyesho ya SIMU EXPO 2016 huku wateja wa Tigo wakifurika


Baadhi ya Wateja wa Kampuni ya Simu Ya Tigo wakiwa katika foleni kwa ajili ya kuhakiki simu zao zoezi linaloendelea kwa ushirikiano baina ya makampuni ya simu na TCRA –CCC leo jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya watoa huduma wa Tigo wakitoa huduma kwa wateja wao wakati wa kampeni ya kuhakiki simu kama ni Bandia au Orijino leo jijini Dar es Slaam.

Meneja Mauzo wa 4G kutoka Tigo Anthony Assenga akisikiliza maoni ya wateja waliotembelea banda la tigo wakati wa kampeni ya kuhakiki simu kama ni Bandi au Orijino leo jijini Dar es Slaam.

Meneja Mauzo wa 4G kutoka Tigo Anthony Assenga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu muitikio wa wananchi katika zoezi la  kuhakiki simu kama ni Bandi au Orijino leo jijini Dar es Slaam.


Watoa huduma wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA – CCC) wakitoa huduma kwa wateja wakati wa kampeni ya kuhakiki simu leo jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wateja wa Kampuni ya Simu ya Tigo akitumbukiza simu yake katika chombp maalulu cha baada ya kubainika kuwa ni simu bandi  alipotemdelea banda la Tigo wakati wa Tamasha la Simu EXPO 2016 leo jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo ni maalumu kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuhakiki simu zao na kudadilisha kabla yakufungiwa ifikapo tarehe 16 mwezi huu.Mteja huyo  alikabidhiwa simu nyingine aina ya Itel 2100 ikiwa na kifurushi cha Dk.550, SMS, 3000 na MB250 kwa gharama ya shilingi elfu 22,000 tu.

Afisa Tawala na Fedha wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania Bi. Amina Ramadhan Haighai akimsaidia mteja aliyetembelea banda lao kufanya uhakiki wa simu kama ni bandia au orijino leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wananchi wakiangalia bidhaa za simu wakati wa Tamasha la Simu EXPO 2016 leo jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo ni maalumu kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuhakiki simu zao na kudadilisha kabla yakufungiwa ifikapo tarehe 16 mwezi huu.Tamasha hilo linafikia tamati kesho sa 11:00 jioni.
Picha na: Frank Shija

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Kumbukumbu la Blogu