Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Kaimu
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania Meja Generali Simon Mumwi wakati wa
hafla uzinduzi wa mashindano ya CDF Cup 2016 jana jijini Dar es Salaam.Kutoka
kulia ni Mkuu wa Utendaji Kivita na Mafunzo, Meja Generali Issa Nassor na Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Alex Nkenyenge.
 |
Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya Maendeleo ya Michezo Alex Nkenyenge (kulia) akiteta jambo na Kaimu Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania Meja Generali Simon Mumwi wakati wa hafla
uzinduzi wa mashindano ya CDF Cup 2016 jana jijini Dar es Salaam.
|
 |
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wanajeshi
wanamichezo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya CDF Cup 2016 jana
jijini Dar es Salaam.Michuano hiyo inatumiwa na Jeshi hilo kutafuta wachezaji
wa Timu ya Taifa ya majeshi itakayoshiriki mashindano ya timu za majeshi Afrika
Mashariki mapema mwezi Agosti Kigali nchini Rwanda.
|
 |
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akimsikiliza kwa makini
Kaimu Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania Meja Generali Simon
Mumwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya CDF Cup 2016 jana jijini Dar
es Salaam.
|
 |
Mkuu wa Utendaji Vitana
na Mafunzo wa Jeshi la Wananchi Tanzania Meja Generali Issa Nassor akizungumza jambo
wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya CDF Cup 2016 jana jijini Dar es
Salaam.
|
 |
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akifurahia onyesho la
grwaride la kimyakimya huku Kaimu
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania Meja Generali Simon Mumwi
(kulia kwake) akimfafanulia jambo jana
jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya CDF Cup 2016.
|
 |
Kikundi cha wanajeshi
kikifanya onyesho la Gwaride la kimyakimya mbele ya Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(hayupo pichani) aliyekuwa
mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa mashindano ya CDF Cup 2016 jana jijini
Dar es Salaam.
|
 |
Wanajeshi wakionyesha
picha ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye
aliyotokana na mchezo wa Kiini macho wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano
ya CDF Cup jana jijini Dar es Salaam.
|
 |
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akionyesha picha yake
aliyokabidhiwa na mmoja wa wanajeshi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano
ya CDF Cup 2016 jana jijini Dar es Salaam.Picha hiyo imetokana na onyesho la
mchezo wa kiini macho.
|
 |
Timu za Brigedi ya Tembo
na JKT zikiingia uwanjani tayari kwa mpambano wa ufunguzi wa mashindano ya CDF
Cup 2016 yaliyonza katika uwanja wa Uhuru jana jijini Dar es Salaam. Michuano
hiyo inatumiwa na Jeshi hilo kutafuta wachezaji wa Timu ya Taifa ya majeshi
itakayoshiriki mashindano ya timu za majeshi Afrika Mashariki mapema mwezi
Agosti Kigali nchini Rwanda.
|
 |
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikagua timu tayari kwa
kuanza kwa pambano la ufunguzi baina ya Timu ya Tembo Brigedi na JKT jana
jijini Dar es Salaam.
|
 |
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa mawaidha kwa
wachezaji wa timu za Tembo Brigedi na JKT kabla ya kuanza pambano lao jana
jijini Dar es Salaam.
|
 |
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja
na wachezaji wa timu za Tembo Brigedi na
JKT kabla ya kuanza pambano lao la ufunguzi wa mashindano ya CDF Cup 2016 jana
jijini Dar es Salaam. Michuano hiyo inatumiwa na Jeshi hilo
kutafuta wachezaji wa Timu ya Taifa ya Jeshi itakayoshiriki mashindano ya timu
za majeshi Afrika Mashariki mapema mwezi Agosti Kigali nchini Rwanda.
Picha na: Frank Shija
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni