Wito
huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,utamadunu,Sanaa na Michezo Bi.Lily Beleko wakati akizungumza na
Waandishi wa habari kuhusu cha maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa Utamaduni Duniani ambapo kauli mbiu ya
madhimisho ya mwaka huu ni” Utamaduni wa Uadilifu na Nidhamu ya Kazi Huleta
Maendeleo”, “Sasa Kazi Tu”.
Kaimu
Mkurugenzi wa Utamaduni Bi.Lily Beleko amesema kuwa ni wajibu kwa kila mtanzania kuheshimu Utamaduni wetu na kushiriki kikamilifu
katika kuutambua, kuujenga,
kuuendeleza na kuurithisha kwa vizazi
vingine.
“Siku
hii ni maalumu kwa kila mtanzaniana na kila mmoja hana budi kukubaliana na
harakati hizi za kulinda, kuhifadhi na kuendeleza Utamaduni wetu kwa ajili ya vizazi
vijavyo”Alisema Bi Lily.
Bi.Lily
Beleko ameongeza kuwa nchi haiwezi
kutambulika na kuheshimika kama Taifa
huru bila kuwa na Utamaduni wake hivyo kuwepo kwa maadhimisho haya kunaipatia
jamii fursa ya kuendelea kukumbushana ,kuhamasishana na kuhimizana katika
kuuenzi utamaduni wa nchi.
Siku
ya Uanuwai wa Utamaduni Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 21 Mei, ambapo
siku hiyo imeteuliwa na Baraza kuu la
Umoja wa Mataifa kuona umuhimu wa kuhifadhi na kuendeleza Utamaduni na hivyo
kupitisha Azimio Na 57/249 mnamo mwaka 2002.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni