JAJI
MKUU: SHERIA YA MITANDAO INA LENGO ZURI
JAJI
MKUU wa Tanzania, Mohammed Chande Othman amesema sheria ya mitandao ilipitishwa
kwa lengo jema la kulinda watumiaji, wanajamii na usalama wa Taifa la Tanzania.
Ametoa
kauli hiyo jana (Jumamosi, Mei 14, 2016) wakati akijibu baadhi ya maswali
kutoka kwa Watanzania waishio Uingereza kwenye mkutano uliofanyika kwenye
Ubalozi wa Tanzania jijini London, Uingereza.
Alisema
watu watatu kati ya wanne nchini Tanzania wakiwemo watoto, wanamiliki simu za
mkononi ambayo ni sawa na watu milioni 35 kati ya milioni 45.
Alisema
sheria hiyo ilitugwa kwa misingi mitatu moja ikiwa ni kumpa mtumiaji uhuru wa
kutoa maoni au taarifa, uhuru ambao alisema unalindwa kikatiba lakini akaonya
kuwa kila uhuru unaotolewa pia una mipaka yake kama ilivyoainishwa kwenye ibara
ya 30(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema
sheria hiyo pia inatoa uhuru wa mtu kuwa na faragha (privacy) na msingi wa tatu
ni sheria hiyo kuzingatia matumizi ya mitandao ili kulinda usalama wa nchi.
“Sheria
hii inakupa uhuru wa kutumia mtandao kumlinda mwanajamii wenzako. Hapa
Uingereza nimeongea na mwendesha mashtaka mkuu ambaye aliniambia kuwa asilimia
60 ya makosa yanayofanyika chini ya sheria ya makosa ya kujamiiana (Sexual
Offencea Act) yanatokana na mitandao,” alisema Jaji Mkuu wakati akijibu swali
kuhusu sheria ya makosa ya mitandao.
Naye
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga alisema kuitishwa kwa mkutano wa
kupambana na rushwa nchini Uingereza ni mojawapo ya jitihada za Waziri Mkuu wa
nchi hiyo kuanzisha vuguvugu la uanaharakati wa mapambano dhidi ya rushwa.
“Kukosekana
kwa utawala bora, changamoto za ugaidi, biashara za dawa za kulevya, biashara
ya kusafirisha binadamu na uwepo wa rushwa na ufisadi ni baadhi ya mambo
yaliyofanya dunia ibadilike. Haya mambo zamani yalikuwa hayana mahali pa
kuzungumzwa, kwa hiyo vikao kama hivi vitasaidia kukabili tatizo hili,”
alisema.
“Rushwa
ni kama pweza mwenye vichwa vingi na mikia mingi. Waziri Mkuu David Cameron
ameamua kuanzisha movement hii ili kutafuta njia za kukabili janga hili kubwa,”
alisema.
Sote
tunatanbua kuwa mataifa mengi yangependa kuwemo katika hii movement lakini ni
faraja kuona kwamba Tanzania imo miongoni mwa waanzilishi na hii ni kwa sababu
ya uongozi nz ujasiri wa Rais Dk. John Pombe Magufuli ambaye kwa kweli ni game
changer (akimaanisha kuwa amebadili
mwelekeo wa Taifa hili) kwani ana utashi wa kisiasa na ana ujasiri wa kukemea
maovu,” alisema huku akishagiliwa
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola alisema vita ya
rushwa nchini Tanzania ni endelevu na inafanyika kuitikia wito alioutoa Rais
Magufuli wakati akizindua Bunge la Tanzania Novemba 20, 2015.
Alisema
wanatumia mbinu mbalimbali kupambana na rushwa lakini kubwa wanayoenda nayo
hivi sasa ni kutoa elimu kwa watoto na vijana ili kuwabadilisha tabia na
utamaduni uliojikita kwenye jamii.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAPILI, MEI 15, 2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni