Tume ya
Vyuo Vikuu Tanzania
TAARIFA
KWA UMMA
MGOGORO WA CHUO KIKUU CHA MT. YOSEFU TANZANIA(SJUIT) KAMPASI YA ARUSHA
1. Tunapenda
kuuarifu
umma
kwamba, Chuo
Kikuu cha Mt. Yosefu
Tanzania (SJUIT) Kampasi ya Arusha ni mojawapo ya vyuo vikuu vilivyosajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ambacho
kilianza kudahili wanafunzi kwa
mara ya
kwanza mwaka wa masomo 2013/2014.
2. Kwa
mujibu wa kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Vyuo Vikuu, Sura ya 346 ya Sheria za Tanzania, Tume ina mamlaka ya kusimamia na kudhibiti ubora na usimamizi wa
uendeshaji
wa Vyuo Vikuu hapa nchini.
3.
Tume inatambua kuwa kwa nyakati
tofauti kumekuwapo na matukio ya
migogoro baina ya uongozi wa Chuo Arusha na wanafunzi. Tume imekuwa
ikifuatilia kwa karibu chimbuko la migogoro hiyo na kuchukua hatua stahiki ikiwa
ni pamoja
na kutoa maelekezo
kwa uongozi wa
chuo kurekebisha kasoro
zinazosababisha migogoro chuoni hapo. Katika kutekeleza azma hiyo, hivi karibuni Tume iliunda jopo la wataalam kufanya ukaguzi wa kina katika Chuo
Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania Kampasi ya Arusha.
Ripoti ya ukaguzi huo
iliwasilishwa tarehe
22/02/2016.
4. Kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa kisheria, ripoti hii inatakiwa kuwasilishwa na kujadiliwa na Kamati ya
Ithibati ya Tume ya Vyuo Vikuu, ambayo itatoa
mapendekezo kwa Tume kuhusu hatua stahiki za maamuzi. Kamati hii itakutana
katika kikao cha dharura tarehe 25/02/2016 saa 3:00 asubuhi, na
taarifa ya
Kamati
hiyo itawasilishwa kwenye
Mkutano wa dharura wa Tume tarehe hiyohiyo saa 9:00 alasiri.
5.
Kwa mantiki hiyo, taarifa rasmi kuhusu maamuzi yaliyofikiwa juu ya hatma ya
Kampasi hiyo ya Arusha ya Chuo cha Mt. Yosefu itatolewa siku ya
Ijumaa tarehe
26/02/2016.
6.
Kwa taarifa hii, Tume inawaomba wanafunzi wote wa Chuo cha Mt. Yosefu
Kampasi ya Arusha kuwa watulivu wakati huu ambapo suala
lao
linashughulikiwa.
7. Tume inapenda
kutumia fursa hii pia
kuwaarifu wanafunzi
wote wa
vilivyokuwa
Vyuo
Vikuu Vishiriki vya Sayansi za Kilimo na Teknolojia (SJUCAST) na Teknolojia
ya
Habari (SJUCIT), kuwa orodha ya
majina yao na vyuo walivyopangiwa inapatikana
katika tovuti
ya Tume ya Vyuo Vikuu.
Hivyo
wanashauriwa
kuondoka Chuoni mara moja na kujiandaa kwa ajili ya kuripoti katika vyuo walivyopangiwa katika muhula wa
pili.
Imetolewa na
PROF.
YUNUS
D. MGAYA
Katibu
Mtendaji
Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania
24 Februari 2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni