Na; Beatrice Lyimo
SHIRIKA
LA Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imerejesha huduma ya upatikanaji wa Maji katika maeneo yote
yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu chini jijini Dar es salaam, pamoja na maeneo ya mji
wa Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na mtambo huo kuzimwa kwa wastani wa saa 36
kuanzia siku ya Alhamisi 18/02/201.
Akizungumzia
kurejea kwa huduma hiyo, Meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro,
amesema kuwa huduma ya Maji katika jiji la Dar es salaam na miji ya Bagamoyo
mkoani Pwani kwa sasa yameanza kwenda kwa wananchi, na maeneo mengi ya jiji ambayo
yalikosa huduma ya Maji kutokana na uzimwaji wa mtambo wa Ruvu chini.
“Napenda
kuwaambia wateja wetu kuwa huduma ya Maji kwa sasa imerejea kwenye maeneo mengi
ya jiji baada ya matengenezo kukamilika na mtambo kuwashwa siku ya Jumapili saa
9:30 alasiri” alisema Bi. Lyaro.
Alibainisha
kuwa Kuna maeneo mengine yatachelewa kupata Maji kwani mara nyingi kwa
kitaalamu huwa mtambo ukizimwa kwa zaidiya saa 24 ndani ya mabomba ya kupitisha
Maji hujaa hewa hivyo baadhi ya maeneo kazi ya utoaji hewa kwenye mabomba
unaendelea, hivyo tuwahakikishie wananchi kuwa huduma imerejea na wataipata
ndani ya muda tuliotarajia.
Awali,
mtambo wa Ruvu Chini ulizimwa ili kuwaruhusu wakandarasi kutoka kampuni ya sino
Hydro na mafundi kutoka DAWASCO kukarabati bomba la Maji lenye inchi 54
linalosafirisha Maji kutoka Bagamoyo mpaka matenki ya Chuo kikuu cha ardhi, Bomba
lililokuwa likivuja maeneo ya Makongo Jeshini, na kusababisha maeneo mbalimbali
ya jiji la Dar es salaam kukosa huduma ya Maji, Mji wa Bagamoyo vijiji vya
Zinga, Kerege na Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani,
Mbezi Beach na Kawe.
Maeneo
mengine ni pamoja na Maeneo ya Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza,
Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo,
City centre, Ilala,, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa
Muhimbili, Buguruni, Chang’ombe na Keko
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni