Jumapili, 21 Februari 2016

Wanafunzi wanaosoma nje ya nchi kusafiri kwa gharama yenye punguzo maalum.

Mwakilishi wa Taasisi ya Sta Travel inayojihusisha na kusafirisha wanafunzi kwa punguzo ya gharama za usafiri Bw. Abbas Karrim akisikiliza maoni kutoka kwa baadhi ya wadau wa elimu waliotembelea meza yake katika maonyesho ya Tanzania Internation Education Fair 2016 yanayoendelea katika Ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

Watanzania wanaosoma masomo ya elimu ya juu nje ya nchi kunufaika na gharama ndogo zenye punguzo maalum za kusafiri wakati wa kwenda na kurudi kutoka masomoni katika nchi wanazo somea kupitia Taasisi ya Sta Travel ya jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa na Mwakilishi wa Taasisi ya Sta Travel Abbass Karim wakati wa monyesho ya Tanzania International Education Fair 2016 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Abbas amesema kuwa taasisi yao imekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania wanaopata fursa ya kusoma nje ya nchi kwani wanatoa huduma ya usafiri ikiwa na punguzo maalum la gharama za usafiri ili waweze kumudu gharama hizo.
Aliongeza kuwa mpaka sasa Taasisi yake imetoa huduma ya hiyo kwa watanzania wengi nhasa wanafunzi wanaoenda kusoma Kuala Lumpar Malyasia, London Uingereza, na Guangzhou China.
Aidha Abbas alisema kuwa pamojja na kutoa huduma hiyo kwa watanzania kumekuwa na changamoto katika upatikanajji wa Viza kwa wateja wao na kupelekea kujitokeza kwa usumbufu, hata hivyo Sta Travel imekuwa ikijitahidi kuwasaidia wateja wake ili wakamilishe taratibu zao kwa wakati.
Kwa upande wake mtanzania aliyenufaika na kupitia Taasisi hiyo Bw. Ally Abdallah amesema kuwa binafsi anaipongeza taasisi hiyo kwa kuwa imemuwezesha kusafirikwa gharama nafuu ambazo kwake zilikuwa rahisi kuzimudu tofauti na gharama halisi ya usafiri kwa kawaida.
Sta Travel ni Taasisi inayojihusisha na utoajji wa huduma ya kusafirisha wanafunzi kwa gharama nafuu yenye punguzo maalum kwa leongo la kuwasaidia watanzania kufikia ndoto zao bila kuwapo na kikwazo.

 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Kumbukumbu la Blogu