(Na
Raymond Mushumbusi-Dodoma)
Serikali
katika kuongeza na kuimarisha uhakika na
usalama wa chakula hapa nchini, Serikali imepanga kujenga maghala 275 kwa awamu
katika sehemu zenye uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi ambapo hadi sasa jumla
ya maghala 125 yanaendelea kujengwa na kukarabatiwa katika maeneo hayo.
Akifafanua
hilo wakati akiharisha shughuli za Mkutano wa Pili wa Bunge la 11 lilikuwa na
vikao 9 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa,Majaliwa amesema Serikali imejipanga katika kuondoa tatizo la upungufu
wa chakula nchini kwa kujenga magala mengi zaidi ya kuhifadhi chakula katika
maeneo mbalimbali yenye changamoto za upungufu wa chakula.
Mhe.
Kassim Majaliwa,Majaliwa amesema hali ya chakula kwa mwaka 2015/2016 katika
maeneo mengi ya nchi imeendelea kuwa ya kuridhisha kufuatia mavuno mazuri
yaliyopatikana msimu wa kilimo wa 2014/2015 na takwimu za Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi zinaonesha kuwa albaki kutoka msimu uliopita nchi ilikuwa na
ziada ya chakula licha ya kuwepo kwa maeneo machache ambayo hayakuwa na
chakula.
“Kutokana na uzalishaji wa mazao
ya chakula kwa msimu wa 2014/2015 kuwa Tani milioni 15.5 na mahitaji ya chakula
kwa mwaka 2015/2016 kuwa Tani milioni 12.9
hivyo nchi imejitosheleza kwa
chakula kwa ziada ya Tani milioni 2.5 sawa na asilimia 120 na napenda
kuwahakikishia Watanzania kuwa Serikali itaendelea kuhudumia maeneo yote yenye
uhaba wa chakula”
“Ili kukabiliana na hali ya uhaba
wa chakula katika maeneo hayo, Serikali inaendelea kutoa chakula katika maeneo
hayo ambapo jumla ya Tani 23,871.6 za
chakula zilitengwa kwa ajili hiyo na hadi kufikia tarehe 17 Januari, 2016,
jumla ya Tani 11,860.8 zilikuwa zimechukuliwa toka Wakala wa Taifa wa Hifadhi
ya Chakula (NFRA) kwenda kwenye Halmashauri za Wilaya zenye upungufu wa chakula
kwa ajili ya usambazaji pia natoa wito kwa Halmashauri ambazo hazijachukua mgao
wao kufanya hivyo mara moja ili Wananchi katika maeneo hayo wasizidi
kuathirika” Alisema Mhe. Majaliwa.
Aidha, Mhe Kassim
Majaliwa,Majaliwa amesema Serikali kwa
kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inaendelea kujenga maghala
ya kimkakati kwa ajili ya kuhifadhi akiba ya Taifa na Kwa sasa ghala moja lenye
uwezo wa kuhifadhi Tani 5,000 limeshajengwa Wilayani
Mbozi Mkoani Mbeya na Serikali imepata mkopo wenye masharti nafuu kutoka
Serikali ya Poland ambao utawezesha kujenga vihenge vya kisasa (silos) vyenye uwezo wa kuhifadhi Tani
160,000 na maghala yenye uwezo wa kuhifadhi Tani 90.
Ameongeza kuwa Pamoja na hatua
zinazochukuliwa na Serikali, amewataka viongozi wa Mikoa, Wilaya na watendaji
katika Halmashauri zote Nchini kuwahamasisha Wananchi kutumia vizuri mvua
zinazonyesha nchini kote kwa kulima kwa bidii ili kuweza kuvuna na kujiwekea akiba
ya chakula cha kutosha kwa ajili ya kaya zao wakati wote wa mwaka na
wawahamasishe wafanyabiashara na wadau wengine kusaidia Serikali kuchukua
chakula kutoka maeneo yenye ziada na kupeleka katika maeneo yenye upungufu na
kwa kuzingatia maelekezo haya pamoja na juhudi za Serikali zilizooneshwa,
tatizo la uhaba wa chakula nchini litapungua, kama siyo kumalizika kabisa.
Waziri Mkuu Mhe Kassim
Majaliwa,Majaliwa amehairisha Mkutano wa Pili Bunge amehairisha shughuli za Bunge
mpaka tarehe 19 mwezi April 2016 saa 3 Asubuhi
likaporejea katika Mkutano wa kujadili Bajeti ya Mwaka wa Fedha
2016/2017.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni