(Na Raymomd Mushumbusi-Dodoma)
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni Mhe Freeman Mbowe Mbunge wa Hai
(CHADEMA) ametangaza rasmi Baraza la Mawaziri vivuli litakalosaidiana na
Serikali katika kuendesha shughuli za kimaendeleo.
Akitangaza Mawaziri hao vivuli kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani
amesema anawaomba Mawaziri wa Wizara husika kuwapa ushirikiano wale wote
walioteuliwa kuwa Mawaziri vivuli katika Kambi ya Upinzani ili kupeleka mbele gurudumu la maendeleo
nchini.
Waliotangazwa Katika Orodha hiyo ni Pamoja na Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na
Utawala Bora Jaffar Michael, Manaibu
wake ni Joseph Nkundi na Ruth Mollel, Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Ali Saleh
Abdalla na Naibu wake ni Pauline Gekul, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Esther Bulaya na Manaibu ni Yusuph Makame na Maftah Abdalla, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ina
mawaziri wawili ambao ni Magdalena Sakaaya na Emmaculate Swari Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Inj. James Mbatia na Naibu Waziri Willy Kombucha.
Aidha ameendelea kuwataja Mawaziri wengine
kuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango Halima
Mdee na Naibu Waziri ni David Silinde,
Waziri wa Nishati na Madini
John Mnyika na Naibu Waziri ni John Heche, Waziri wa Katiba na Sheria Tundu Lissu na Naibu Waziri Abdalla Mtolela, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Peter Msigwa na Naibu Waziri Riziki Shaghal, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Juma Omari na Naibu Waziri Mwita Waitara, Waziri ya Mambo ya Ndani Godbless Lema na Naibu Waziri Masoud Abdalla, Waziri ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilfred Lwakatare na
Naibu Waziri Salum Mgoso.

Wengine walioteuliwa katika Baraza kivuli ni Waziri wa Maliasili na Utalii Esther
Matiko na Naibu Waziri Cecilia Pareso, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Anthony Komu na Naibu
Waziri Cecil Mwambe, Waziri wa
Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi Suzan Lyimo Naibu Waziri Dkt. Ali
Suleiman Yusuph, Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel na Naibu
Waziri Zubeda Sakul, Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Joseph Mbilinyi na Naibu Waziri
Devotha Minja na Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Hamidu Hassan na Naibu Waziri Peter Lijualikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni