Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.
Joyce Fissoo (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya Bodi ya Filamu
na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mukandala Lufufu
inayojishughulisha na kazi ya kutafsiri Filamu kwa Lugha ya Kishwahili
Bw. Derick Mukandala maarufu kwa jina la Mzee Lufufu.(kulia) katika ni Afisa
Utamaduni kutoka Bodi ya Filamu Bw.Benson Mkenda
Habari/Picha na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mukandala Lufufu inayojishughulisha na kazi ya kutafsiri
Filamu kwa Lugha ya Kishwahili Bw. Derick Mukandala maarufu kwa jina la Mzee
Lufufu amekiri kuwa kazi yake anaifanya kienyeji ili hali akifahamu ni makosa.
Kauli hiyo ameitoa jana katika kikao baina yake na
Bodi ya Filamu ambapo alieleza kuwa amekuwa akifanya kazi hiyo kwa muda mrefu
bila kuzingatia utaratibu huku akijua kuwa ni makosa kwa mtu kutumia kazi ya
msanii mwingine bili idhini yake.
“Nikiri tu kwamba nimekuwa nikifanya makosa kwa
kutafsiri Filamu bila kuwa na idhini ya wahusika wa filamu hizo” Alisema
Lufufu.
Mzee Lufufu aliongeza kuwa amekuwa akifanya kazi
hiyo ya kutafsiri Filamu bila vibali akiamini kuwa hakuna ubatili wowote.
Aidha Mzee Lufufu pamoja na kujua ni makosa
kutafsiri Filamu bila idhini alikuwa anatarajia kufanya kazi na Kampuni moja ya
kutoka nchini Norway ambapo kama amngefanikiwa kufanya Documentary ambayo
ingejulikana kwa jina la “The Film Dubber
from Dar es Salaam – Mzee Lufufu” hiyo ingeaminisha ulimwengu kuwa Tanzania
inaruhusu uharamia wa kazi za wasanii kitu ambacho siyo sahihi.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa siyo dhambi kutafsiri Filamu, ila ni lazima
anayetaka kufanya kazi hiyo azingatie dheria za nchi na taratibu zinaotakiwa
kuzingatiwa.
Fissoo amesema kuwa sheria ya Filamu nchini kifungu
namba 17 kinamtaka anayetaka kufanya kazi ya kutafsiri awasilishe muswada wake
katika ofisi za Bodi ya Filamu ili uhakikiwa na wataalamu kabla ya kupewa
idhini ya kuendelea na kazi hiyo.
Aliongeza kuwa ili kazi ya kutafsiri Filamu ni
sharti mhusika kupata idhini ya mwenye Haki Miliki ya filamu husika hivyo ni vyema
kuwasiliana na COSOTA ili kufanya utaratibu wa kupata uhalali akitolea mfano wa
Filamu ya Nelia iliyotengenezwa nchini Zimbabwe na baadaye ilifanyiwa tafsiri
katika lugha ya Kiswahili hapa jijini Dar es Salaam baada ya kufuata taratibu
zote.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni