Jumapili, 2 Desemba 2018

Rais Dkt. Magufuli Aweka Jiwe la Msingi Mradi Mkubwa wa Maji Katika Jiji la Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Maji safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Isaack Kamwelwe pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira utakaosaidia jiji la Arusha katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Kimyaki Arumeru mkoani Arusha.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia maji yanayotoka katika moja ya visima virefu vilivyopo katika mradi huo mkubwa wa maji safi na usafi wa mazingira katika jiji la Arusha. Mradi huo utakapokamilika utaweza kuzalisha lita za ujazo milioni 200  kwa siku tofauti na sasa ambapo lita za ujazo ni 45 milioni wakati mahitaji ya jiji la Arusha ni lita za ujazo milioni 90.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru wakati wa mkutano na wananchi wa Arumeru jijini Arusha mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Arumeru mara baada ya kuweka  jiwe la msingi mradi wa Maji safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha

Wananchi wa Arumeru wakishangilia wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kijiji cha Kimnyaki Arumeru.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati akiondoka katika eneo la mkutano.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Meya wa jiji la Arusha Calist Lazaro mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Arumeru. PICHA NA IKULU






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Kumbukumbu la Blogu