Doris ambaye pia ni mshindi wa tatu wa Redds Miss
Tanzania 2014 ni mwanaharakati wa dhana ya Urembo wenye Malengo endelevu kwa
jamii ‘Beauty with a Purpose’. Amefanya
kazi kubwa kwenye sekta ya elimu akijikita zaidi kwenye kuchangia Vitabu kwa shule
za msingi na sasa, akiwa ni mmoja ya watu ambao walizaliwa kabla ya muda wa
kawaida ameamua kupanua wigo wake wa huduma za jamii kuleta mwamko na kusaidia
kuokoa maisha ya watoto hawa.
Akiongea kwenye hafla ya kukabidhi mashine hizo
iliyofanyika hospitalini hapo, Mollel alisema. “Kiwango cha vifo kwa watoto
wanaozaliwa kabla ya kukomaa ni karibu 30% vikichangiwa kwa kiasi kikubwa na
ukosefu wa vifaa vya kutosha kusaidia mifumo yao ya upumuaji mara tu
wanapozaliwa. Nikiwa moja ya watoto hao ambaye nilibahatika kupata msaada na
huduma ya kutosha nilipozaliwa, Ninaelewa ni jinsi gani matunzo haya ya awali
yalivyo muhimu kwenye kuokoa maisha ya watoto hawa na ninajikita kuwasaidia”
Bw. Albert Mbepera, Mkurungezi wa Albert Manifester
Photojournalism; kitengo ndani ya Manifester brand kilichojikita kwenye masuala
ya jamii alisema ‘huduma kwa jamii ni eneo muhimu sana kwetu. Tunafurahi
kujitolea kufanya kazi na Doris katika maswala ya kusaidia jamii na tunaamini
kuwa ushirikiano huu utasaidia kukusanya na kuonyesha matatizo ya wahitaji ili
kuongeza uelewa na msukumo wa misaada kutoka kwa sekta binafsi na wanajamii kwa
ujumla’
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni mkuu wa
wilaya ya Singida Bi Queen Mlozi na ilihudhuriwa na Mganga mfawidhi wa
hospitali ya mkoa wa Singida Bw. Daniel Tarimo, Daktari bingwa wa watoto wa
Hospitali ya Singida, Muandaaji wa Redds Miss Singida 2014 Bora Lemmy na
washindi wengine wa Redds Miss central Zone Linda Bureta, blath Chambia, Suzy
Wahere.
Doris Mollel na Manifester brand wanapenda
kuwashukuru ANUDHA PHARMACEUTICALS LTS kwa mchango wao mkubwa katika
kufanikisha shughuli hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni