|
Afisa Uchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni
na Michezo ,Bw.Yohana Ngao akiwa katika majadiliano na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri
ya Mtwara Vijijini Bw.Oscar Ng’itu ilikujua maoni na changamoto wanazopata wana
vikundi waliopata mkopo kupitia mfuko wamaendeleo yaVijana katika eneo lake.
Picha na Daud Manongi
Kikundi
cha Vijana cha AMKENI kutoka katika Halmshauri ya Manispaa ya Mtwara kimefanikiwa kujiajiri na
kuutumia vyema mkopo waliopewa na Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo
ili kuanzisha miradi mbalimbali waliyoomba kupitia mfuko wa Maendeleo ya
Vijana.
Hayo
yamesemwa leo na katibu wa kikundi cha AMKENI kilichopo chini ya saccos ya
Halmashauri ya Mtwara Vijijini Bw.Iddi Saidi Dogoa alipokuwa akiwaeleza wajumbe
wa Kikosi kazi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo
walipowatembelea ili kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mfuko wa Maendeleo ya
Vijana wilayani hapo.
Kikundi
hicho kinajishughulisha na ubebaji wa mizigo na kilimo na walipewa shilingi
milioni saba ili kufanikisha mradi huo.”tumefurahi sana kupata mkopo kutoka
Serikalini,kwani umetuwezesha kujiajiri na hata kuajiri watu wengine na pia
tumeweza kulipa kodi ili kuchangia maendeleo ya Taifa letu”Aliongeza Bw. Iddi.
Aidha
kikundi cha AMKENI kimefanikiwa kutumia vyema pesa inayopatikana kama faida
kujiendeleza zaidi kimaisha kwani wameweza kununua viwanja na sasaivi
wanakikundi wana sehemu za kuishi binafsi,wanajiandaa pia kuanza kilimo cha
mihogo kupitia faida waliyopata katika biashara zao za kila siku.
Naye
Kaimu Mkurugenzi Halmshauri ya manispaa ya mtwara Bw.Rashid Mohamed ameshauri serikali kuendelee
kujenga utaratibu wa kusaidia vijana wasio na kazi rasmi ili kuepukana na bomu
la ajira kwa Vijana,na pia mikopo hii iwe chini ya masharti ya benki ili
kuiboresha zaidi ili marejesho yafanywe kwa wakati.
Aidha
Katibu msaidizi wa kikundi cha vijana saccos(MTWAYODEN),BwMohamed Ngowe
ameishukuru Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kwa kuwatembelea na
kujua matatizo na changamoto wanazopata ili kuwapatia suluhisho na kukazia kuwa
Wizara iendelee kutoa mikopo hii kwa wakati ili Vijana zaidi wazidi kuona na
wavutiwe kujiunga.
Mfuko
wa maendeleo ya Vijana ulianzishwa Chini ya Sheria Na.21 ya mwaka 1961 kifungo
cha 17(1) ukiwa na lengo la kuwasaidia Vijana kupata mikopo yenye masharti
nafuu na kuwajengea uwezo kiuchumi ili waweze kuanzisha au kuimarisha miradi
yaokwa lengo la kuwawezesha kujitegemea na kukuza uchumi wa nchi.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni