Ijumaa, 28 Aprili 2023

COSTECH YAKUTANISHA BUNIFU 50 DODOMA

 

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari lipotembelea mabanda katika maonesho ya ubunifu yanaendelea kufuatia Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Kitaifa (IWTZ)  jijini Dodoma. Maaadhisho hayo yamefanyika katika uwanja wa Jamhuri yakiwa na kauli mbiu “Ubunifu kwa Uchumi Shindani”.( Picha na Paschal Nkwabi)


 COSTECH YAKUTANISHA BUNIFU 50 DODOMA

Na: Paschal Nkwabi, DODOMA

Tume ya Taifa ya Sayansis na Tekeknolojia (COSTECH) imealika bunifu 50 inazoziratibu kuonesha kiwanago cha hatua walizofika kwenye ubunifu wao kwaajili ya kukabiliana na  mahitaji mbalimbali ya shughuli za watanzania. 

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu aliokuwa akuizungumza na waandishi wa habari wakati wakutembelea mabanda ya maonesho wa wabunifu (MAKISATU) kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Kitaifa (IWTZ)  katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma..

Dkt. Nungu amesema kuwa COSTECH ambayo ndiyo yenye dhamana ya la kuratibu maendeleo ya sayansi na tekenolojia imechagua bunifu 50 ambazo zinaendelezwa na ziko kwenye taasisi mbalimbali ili kazi zao zionekane kwa wananchi na wadau wa maendeleo ya  sayansi teknolojia  na ufundi kuziona.

Aliongeza kuwa kupitia maonesho hayo wabunifu watapata fursa ya kupata mrejesho kutoka kwa wadau mbalimbali wanaotembelea maonesho hayo ambapo watafanya tathmini jambo litakalosaidia kufanya maboresho kwa lengo la kuendana na viwangi vya ubora vinavyohitajika kabla ya kuanza uzalishaji wa kibiashara.

“Maonyesho haya yanatija kwa bunifu za hapa nyumbani kwani kupitia MAKISATU kuna ondoa ile fikra iliyomo ndani ya baadhi ya watanzania kuwa vumbuzi na bunifu zao hazithaminiwi na kuendelezwa jambo ambalo si sawa”, alisema Dkt. Nungu.

Aidha Dkt. Nungu ametolea mfano wa bunifu iliyofanywa na wazo  wabunifu ambao bidhaa zao zimefikia hatua ya  utengenezwaji kwa ajili ya uuzwaji ikiwemo mfumo wa kuhesabu matumizi ya maji uliokubaliwa na Mamlaka ya Maji ya Arusha.

“Baaadhi ya bunifu tulizotembelea kwenye maonesho hayo mfano Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wabunifu kutoka chuo hicho wamekuja na teknolojia ya uzalishaji wa nishati mbadala wa mafuta inayotengenezwa kwa kutumia ndizi ambayo inaweza kuwasha kibatari na pia injini.” Alisema Dkt. Nungu.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Lewis Mutashobya amesema kuwa utafiti huo ukifikia kiwango cha mwisho unaweza kutumiwa na wananchi wengi hasa vijiji ambako ndizi zinapatikana kwaajili ya chanzo mbadala cha nishati.

Katika maonesho hayo baadhi ya washiriki akiwemo Bw. Zomokunk Thwala  kutoka nchini Afrika Kusini ambaye aliyekuja kuonesha bidhaa zake kwenye maonesho hayo amesema kuwa amefurahishwa kuona jinsi Tanzania na Afrika inavyojipambanua kwenye uwekezaji wa sayansi na teknolojia.

Mbali na bunifu hizo zipo bidhaa nyingine za ubunifu kwenye kilimo, ujenzi , usindikajiwa mazao elimu, uselemala electroniki  na teknolojia ya habari ambazo Mkurugenzi huyo ameomba watanzania kuzithamini na kuwaamaini wabunifu wake.

Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Taifa (IWTZ) yanasimamiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ambapo mwaka huu kauli mbiu yake ni “Ubunifu kwa Uchumi Shindani”.

Mwisho

Jumapili, 25 Oktoba 2020

Wasimamizi Vituo vya Kupigia Kura Jimbo la Shinyanga Mjini Wapigwa Msasa

Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Bw. Fabian Kamoga akifafanua jambo wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Shinyanga Mjini leo tarehe 25 Oktoba 2020. Jimbo la Shinyanga Mjini lina jumla ya vituo vya kupigia kura 326 ambapo wasimamizi wa vituo vyote na wasaidizi wao wameshiriki mafunzo hayo.


Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Bw. Fabian Kamoga akifafanua jambo wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Shinyanga Mjini leo tarehe 25 Oktoba 2020. Jimbo la Shinyanga Mjini lina jumla ya vituo vya kupigia kura 326 ambapo wasimamizi wa vituo vyote na wasaidizi wao wameshiriki mafunzo hayo.

Msimamizi Msadizi wa Uchaguzi Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini, Bw. Rajab Massanche akizungumza wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Shinyanga Mjini leo tarehe 25 Oktoba 2020. Jimbo la Shinyanga Mjini lina jumla ya vituo vya kupigia kura 326 ambapo wasimamizi wa vituo vyote na wasaidizi wao wameshiriki mafunzo hayo.Kutoka kushoto ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Lubaga, Bw. Lucas Venance na Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Bw. Fabian Kamoga (katikati).


Afisa Uchaguzi wa Manispaa ya Shinyanga, Bw.Charles Kafutila akielezea jambo wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Shinyanga Mjini leo tarehe 25 Oktoba 2020. Jimbo la Shinyanga Mjini lina jumla ya vituo vya kupigia kura 326 ambapo wasimamizi wa vituo vyote na wasaidizi wao wameshiriki mafunzo hayo.

Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika Kata za Chamaguha na Kizumbi, Bi. Jesca Kipingu na Bw. Mwombeki Gadios wakitoa maelezo ya namna ya kufunga sanduku la kupigia kura wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Shinyanga Mjini leo tarehe 25 Oktoba 2020. Jimbo la Shinyanga Mjini lina jumla ya vituo vya kupigia kura 326 ambapo wasimamizi wa vituo vyote na wasaidizi wao wameshiriki mafunzo hayo.

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Ibinzamata, Bw. Victor Kajuna akitoa maelezo ya moja ya kifaa kinachotumika katika kituo cha kupigia kura wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Shinyanga Mjini leo tarehe 25 Oktoba 2020. Jimbo la Shinyanga Mjini lina jumla ya vituo vya kupigia kura 326 ambapo wasimamizi wa vituo vyote na wasaidizi wao wameshiriki mafunzo hayo.

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata Kizumbi, Bw. Mwombeki Gadios akitoa maelekezo ya jinsi ya kufunga sanduku la kupigia kura wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Shinyanga Mjini leo tarehe 25 Oktoba 2020.Jimbo la Shinyanga Mjini lina jumla ya vituo vya kupigia kura 326 ambapo wasimamizi wa vituo vyote na wasaidizi wao wameshiriki mafunzo hayo.


Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura wakifuatilia mada wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Shinyanga Mjini leo tarehe 25 Oktoba 2020. Jimbo la Shinyanga Mjini lina jumla ya vituo vya kupigia kura 326 ambapo wasimamizi wa vituo vyote na wasaidizi wao wameshiriki mafunzo hayo. (Na Mpiga Picha wetu, Shinyanga)


 

Jumanne, 18 Februari 2020

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Yapongezwa Uandaaji Bajeti

Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje toka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Robert Mtengule akiongoza kikao cha mapitio ya Bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) leo jijini Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Masajili wa Vyama vya Siasa, F. Mazone akizungumza wakati wa kikao cha mapitio ya Bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) leo jijini Dodoma. Kulia ni Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje toka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Robert Mtengule.

Afisa Usimamizi wa Fedha(FMO) kutoka Wizara ya Fedha na Mipango,Bw. Ezekiel Odipo ambaye pia ni Msimamizi wa Dawati la Bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa akichangia mada wakati wa kikao cha mapitio ya Bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) leo jijini Dodoma. 

Baadhi ya wajumbe Kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya Mwaka 2020/2021 toka ofisi hiyo wakifuatilia maoni ya Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje toka Wizara ya Fedha na MipangoBw. Robert Mtengule  katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ORPP jijini Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Mapitio ya Makadirio ya Bajeti ya Mwaka 2020/2021 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) toka Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia maoni ya Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje toka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Robert Mtengule (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ORPP jijini Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Mapitio ya Makadirio ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) na Wizara ya Fedha wakifuatilia maoni ya Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje toka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Robert Mtengule (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ORPP jijini Dodoma.Kikao hicho kimehusisha wajumbe kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Wizara ya Fedha na Mipango.  (Picha na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa - ORPP)

Jumatano, 26 Juni 2019

Serikali Yaja na Suluhisho la Walanguzi wa Tiketi za Mabasi

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kuanza kwa majaribio ya Mfumo wa kukata tiketi kwa njia ya Tehama leo Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA), Gilliard Ngewe na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Emmanuel Stephen Ndomba. Majaribio hayo yanaanza leo tarehe 26 Juni 2019 katika njia itakayoanishwa kabla ya kuanza kutumika nchi nzima.

Afisa Habari wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta kuu ya Uchukuzi), Christopher Phillemon akitoa maelezo mafupi kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia) kuhusu kuanza kwa majaribio ya Mfumo wa kukata tiketi kwa njia ya Tehama leo Jijini Dodoma.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA), Gilliard Ngewe. Majaribio hayo yanaanza leo tarehe 26 Juni 2019 katika njia itakayoanishwa kabla ya kuanza kutumika nchi nzima.

Baadhi ya Waandoshi wa Habari wakifutilia maelezo ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe kuhusu kuanza kwa majaribio ya Mfumo wa kukata tiketi kwa njia ya Tehama leo Jijini Dodoma. Majaribio hayo yanaanza leo tarehe 26 Juni 2019 katika njia itakayoanishwa kabla ya kuanza kutumika nchi nzima.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akisikiliza kwa makini swali kutoka kwa Waandishi wa Habari wakati wa mkutano wake na waandishi hao (hawapo pichani) kuhusu kuanza kwa majaribio ya Mfumo wa kukata tiketi kwa njia ya Tehama leo Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA), Gilliard Ngewe na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Emmanuel Stephen Ndomba. Majaribio hayo yanaanza leo tarehe 26 Juni 2019 katika njia itakayoanishwa kabla ya kuanza kutumika nchi nzima.

Afisa Habari wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta kuu ya Uchukuzi), Christopher Phillemon akiwa na baadhi ya Waandishi wa Habari wakifutilia maelezo ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (hayupo pichani) kuhusu kuanza kwa majaribio ya Mfumo wa kukata tiketi kwa njia ya Tehama leo Jijini Dodoma. Majaribio hayo yanaanza leo tarehe 26 Juni 2019 katika njia itakayoanishwa kabla ya kuanza kutumika nchi nzima.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akiagana na Waandishi wa Habari baada ya kumaliza mkutano wake na waandishi hao kuhusu kuanza kwa majaribio ya Mfumo wa kukata tiketi kwa njia ya Tehama leo Jijini Dodoma. Majaribio hayo yanaanza leo tarehe 26 Juni 2019 katika njia itakayoanishwa kabla ya kuanza kutumika nchi nzima. (Na: Mpiga Picha Wetu)


Prof. Kabudi Ahudhuria Mkutano wa Waratibu wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Afrika (FOCAC)


RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. SHEIN AKITOA MKONO WA POLE KWA FAMILIA YA DR. BADRIA NA KUHUDHURIA HITMA MASJID MAAMUR UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitoa mkono wa Pole kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodo alipofika nyumbani kwao Mtaa wa Msasani Jijini Dar es Salaam kutowa Mkono kwa familia ya Dr. Badria. Abubakar Gurnah 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwafariji Watoto wa Marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah, alipofika nyumbani kwao kutowa mkono wa pole na kuwafariji kwa msiba huo, katikati Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibae Dr. Abdalla Juma Mabodi mume wa Marehemu Dr.Badria Abubakar Gurnah.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,. Dk. Ali Mohamed Shein, akisaini kitabu cha maombolezi cha Marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah, alipofika nyumbani kwao Msasani Jijini Dar es Salaam kutowa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, akisaini kitabu cha maombolezi alipofika nyumbani kwa marehemu Dr. Badria Abubakari Gurnah, Msasani Jijini Dar es Salaam

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akimfariji Mtoto wa Marehemu Zaina Abdalla Juma Mabodi, alipofika nyumbani kwao Msasani Jijini Dar es Salaam, kutoa mkono wa pole, kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr, Abdalla Juma Mabodi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akimfariji Mtoto wa Marehemu Zaina Abdalla Juma Mabodi, alipofika nyumbani kwao Msasani Jijini Dar es Salaam, kutoa mkono wa pole, kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr, Abdalla Juma Mabodi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein , kulia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr, Abdalla Juma Mabodi, wakiitikia dua kumuombea Marehemu Dr.Badria Abubakar Gurnah, alipofika nyumbani kwao Msasani kutowa mkono wa pole.

MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushoto Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na kulia Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi wakishiriki katika hitama na dua  ya kumuombea Marehemu Dr.Badria Abdubakar Gurnah, iliofanyika nyumbani kwao Msasani Jijini Dar es Salaam.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi Jijini Dar es Salaam, katika hitma na dua kumuombea marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah, iliofanyika nyumbani kwao Msasani Dar es Salaam.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akipiga fatha kabla ya kuaza kwa kisoma cha dua na hitma ya kumuombea marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah, iliofanyika katika Masjid Mahamur Upanga Jijini Dar es Salaam, kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar mume wa marehemu Dr, Abdalla Juma Mabodi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akishiriki katika kisoma cha Hitma na dua kumuombea Marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah, kushoto Imamu wa Masjid Mahamur Upanga Sheikh Ayoub Ali Seif na Sheikh Zeni Shariff na kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ramadhani Abdalla.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na kushoto Imamu wa Masjid Mahamur Upanga wakiitikia dua wakati wa kuhitimisha Hitma ya marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah ikihitimishwa na Sheikh Zeni Shariff.


Jumanne, 25 Juni 2019

KAMISHNA WA UHIFADHI TANAPA,DKT ALLAN KIJAZI AWAVISHA VYEO ASKARI UHIFADHI WAKUU NA WAANDAMIZI


Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akikagua Gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya programu ya kuvalisha Vyeo Askari Uhifadhi Wakuu na Askari Waandamizi .
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),Dkt Allan Kijazi akipokea saluti kutoka kwa kiongozi wa  Brass Bendi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)  mara baada ya kufanya ukaguzi.
  
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt, Allan Kijazi akiongozwa kuelekea katika Jukwaa mara baada ya kuhitimisha zoezi la ukaguzi kwa askari wa Uhifadhi wakati wa Gwaride Maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya programu ya kuvalisha Vyeo Askari Uhifadhi Wakuu na Askari Waandamizi .

Askari Uhifadhi Wakuu na Askari Waandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakila kiapo cha utii wakati wa programu ya kuvalisha Vyeo Askari Uhifadhi Wakuu na Askari Waandamizi iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mto wa Mbu katika wilaya ya Monduli..

Brass Band ya  Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikiongoza Gwaride Maalumu kutoka nje ya uwanja.
Gwaride likitoka nje ya Uwanja.


Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akiwavisha vyeo vipya vya kijeshi Askari Waandamizi wa shirika hilo programu iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mto wa Mbu wilayani Monduli. 


Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akiwavisha vyeo vipya vya kijeshi Askari Wakuu wa shirika hilo programu iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mto wa Mbu wilayani Monduli.


Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akizungumza mara baada ya kuwavisha vyeo vipya vya kijeshi Askari Wakuuu na Askari Waandamizi wa shirika hilo programu iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mto wa Mbu wilayani Monduli.


Baadhi ya Makamishna Wasaidizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) pia walikuwa ni miongoni mwa walioshuhudia uvishwaji huo wa vyeo vipya kwa Askari Wakuu na Askari Waandamizi .


Naibu Kamishna-Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara TANAPA ,William Mwakilema akizungumza wakati wa hafla hiyo.


Naibu Kamishna wa Uhifadhi -Fedha na Rasilimali watu -TANAPA, Nassoro Mndeme akizungumza wakati wa zoezi la uvishaji vyeo vipya kwa Askari Uhifadhi Wakuu na Waandamizi.


Baadhi ya Makamishna Wasaidizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) pia walikuwa ni miongoni mwa walioshuhudia uvishwaji huo wa vyeo vipya kwa Askari Wakuu na Askari Waandamizi .


Kamishna wa Uhifadhi Msaidizi Mwandamizi Mawasiliano TANAPA,Pascal Sheletete akitoa maelezo ya namna ya zoezi la upigaji picha za pamoja litafanyika.

Mgeni Rasmi Kamishna Uhifadhi (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na Askari Wakuu mara baada ya kuvikwa vyeo vipya . 


Mgeni Rasmi Kamishna Uhifadhi (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna Uhifadhi Wasaidizi Waandamizi mara baada ya baada ya kuwavisha  vyeo vipya kwa Askari  Uhifadhi Wakuu na Waandamizi .
Askari Uhifadhi  Wakuu na Waandamizi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuapishwa na kuvikwa vyeo vipya.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi TV.

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Kumbukumbu la Blogu