Ijumaa, 28 Aprili 2023

COSTECH YAKUTANISHA BUNIFU 50 DODOMA

 

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari lipotembelea mabanda katika maonesho ya ubunifu yanaendelea kufuatia Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Kitaifa (IWTZ)  jijini Dodoma. Maaadhisho hayo yamefanyika katika uwanja wa Jamhuri yakiwa na kauli mbiu “Ubunifu kwa Uchumi Shindani”.( Picha na Paschal Nkwabi)


 COSTECH YAKUTANISHA BUNIFU 50 DODOMA

Na: Paschal Nkwabi, DODOMA

Tume ya Taifa ya Sayansis na Tekeknolojia (COSTECH) imealika bunifu 50 inazoziratibu kuonesha kiwanago cha hatua walizofika kwenye ubunifu wao kwaajili ya kukabiliana na  mahitaji mbalimbali ya shughuli za watanzania. 

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu aliokuwa akuizungumza na waandishi wa habari wakati wakutembelea mabanda ya maonesho wa wabunifu (MAKISATU) kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Kitaifa (IWTZ)  katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma..

Dkt. Nungu amesema kuwa COSTECH ambayo ndiyo yenye dhamana ya la kuratibu maendeleo ya sayansi na tekenolojia imechagua bunifu 50 ambazo zinaendelezwa na ziko kwenye taasisi mbalimbali ili kazi zao zionekane kwa wananchi na wadau wa maendeleo ya  sayansi teknolojia  na ufundi kuziona.

Aliongeza kuwa kupitia maonesho hayo wabunifu watapata fursa ya kupata mrejesho kutoka kwa wadau mbalimbali wanaotembelea maonesho hayo ambapo watafanya tathmini jambo litakalosaidia kufanya maboresho kwa lengo la kuendana na viwangi vya ubora vinavyohitajika kabla ya kuanza uzalishaji wa kibiashara.

“Maonyesho haya yanatija kwa bunifu za hapa nyumbani kwani kupitia MAKISATU kuna ondoa ile fikra iliyomo ndani ya baadhi ya watanzania kuwa vumbuzi na bunifu zao hazithaminiwi na kuendelezwa jambo ambalo si sawa”, alisema Dkt. Nungu.

Aidha Dkt. Nungu ametolea mfano wa bunifu iliyofanywa na wazo  wabunifu ambao bidhaa zao zimefikia hatua ya  utengenezwaji kwa ajili ya uuzwaji ikiwemo mfumo wa kuhesabu matumizi ya maji uliokubaliwa na Mamlaka ya Maji ya Arusha.

“Baaadhi ya bunifu tulizotembelea kwenye maonesho hayo mfano Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wabunifu kutoka chuo hicho wamekuja na teknolojia ya uzalishaji wa nishati mbadala wa mafuta inayotengenezwa kwa kutumia ndizi ambayo inaweza kuwasha kibatari na pia injini.” Alisema Dkt. Nungu.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Lewis Mutashobya amesema kuwa utafiti huo ukifikia kiwango cha mwisho unaweza kutumiwa na wananchi wengi hasa vijiji ambako ndizi zinapatikana kwaajili ya chanzo mbadala cha nishati.

Katika maonesho hayo baadhi ya washiriki akiwemo Bw. Zomokunk Thwala  kutoka nchini Afrika Kusini ambaye aliyekuja kuonesha bidhaa zake kwenye maonesho hayo amesema kuwa amefurahishwa kuona jinsi Tanzania na Afrika inavyojipambanua kwenye uwekezaji wa sayansi na teknolojia.

Mbali na bunifu hizo zipo bidhaa nyingine za ubunifu kwenye kilimo, ujenzi , usindikajiwa mazao elimu, uselemala electroniki  na teknolojia ya habari ambazo Mkurugenzi huyo ameomba watanzania kuzithamini na kuwaamaini wabunifu wake.

Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Taifa (IWTZ) yanasimamiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ambapo mwaka huu kauli mbiu yake ni “Ubunifu kwa Uchumi Shindani”.

Mwisho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Kumbukumbu la Blogu