JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
IKULU
Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Septemba, 2016
amemteua Bw. Ado Steven Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.
Bw. Ado Steven
Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Benedict Richard Ole Kuyan
ambaye amestaafu.
Pia, Rais Magufuli
amemteua Bw. Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.
Bw. Tixon Tuliangine
Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Symthies Emmanuel Pangisa ambaye
amestaafu.
Tarehe ya kuapishwa
kwa Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa itatangazwa baadaye.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
09 Septemba, 2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni