 |
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt (mwenye nguo nyekundu) akisalimiana na
Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga mara baada ya kuwasili katika ofisi
za Shirika hilo zilizopo Tengeru jijini Arusha alipoenda kuzindua mradi wa
BEYOND 2015 juzi
|
 |
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt (mwenye nguo nyekundu) akisikiliza maelezo
mafupi kuhusu Shirika lisilo la Kiserikali la DSW Tanzania kutoka kwa
Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Peter Owaga mara baada ya kuwasili katika ofisi
za Shirika hilo zilizopo Tengeru jijini Arusha juzi.Wa mwisho kushoto ni Mkuwa
Wialaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe Munasa
|
 |
Mkurugenzi wa DSW
Tanzania Bw. Peter Owaga akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi
wa BEYOND 2015 juzi jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Mke wa Rais wa Shirikisho
la Ujerumani Bibi. Daniela Schadt, Mke wa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania
Bibi. Wenday Marshall – Kochanke na Mratibu wa Programu za Vijana kutoka Wizara
ya Afya, na Ustawi wa Jamii Dkt. Elizabeth Mapella. BEYOND 2015 ni mradi
uliolenga kuongeza hamasa na ushawishi kwa wadau wa maendeleo kutoa kipaumbele
kwa vijana husasni katika Elimu, Afya ya uzazi na Ajira.
|
 |
Baadhi ya washiriki wa
hafla ya uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015 wakimsikiliza Mkurugenzi wa DSW
Tanzania Bw. Peter Owaga (hayupo pichani).
|
 |
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akiteta jambo na
Mkurugenzia wa DSW Tanzania(katikati) pamoja na Mratibu wa Mradi wa BEYOND 2015
Bi. Esther Mwanjesa mara baada ya kuzindua mradi huo juzi jijini Arusha.
|
 |
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akifuarahi mara baada
ya kukata utepe na kuzindua rasmi mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini
Arusha.Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa DSW Tanzania ambao ndiyo watekelezaji wa
mradi huu Bw. Peter Owaga. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe
Munasa (nyuma ya Mke wa Rais wa Ujerumani) na Mratibu wa Mradi huo Bi. Ester
Mwanjesa aliyeshika kitabu.
|
 |
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt(mwenye nguo nyekundu)
akisikiliza maelezo kuhusu mradi wa BEYOND 2015 kutoka kwa Mratibu wa mradi huo
Bi. Esther Mwanjesa (kushoto) kabla ya kuzindua rasmi mradi huo juzi jijini
Arusha. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga na
kushoto kwa Mke wa Rais wa Ujerumani ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe
Munasa.
|
 |
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akipokea zawadi ya Kimasai
kutoka kwa Mwanamke mjasiriamali Bibi.Salome Samwel wakati alipotembelea
maonyesho ya biaadha zao katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa mradi wa BEYOND
2015, juzi jijini Arusha.
|
 |
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akivaa heleni alizopewa
kama zawadi kutoka kwa Mwanamke wa mjasiriamali Bibi.Salome Samwel wakati
alipotembelea maonyesho ya bidhaa zao yaliyokuwa katika hafla ya uzinduzi wa
mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini Arusha.
|
 |
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt na Mwanamke mjasiriamali mwenye asili ya
Kimasai Bibi.Salome Samwel wakiwa katika nyuso za furaha juzi jijini Arusha
wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015 unaoratibiwa na kutekelezwa
na DSW Tanzania.
|
 |
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akiangalia zawadi ya michoro ya kitamaduni aliyopewa na
Shirika la DSW Tanzania wakati wa hafla uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015 juzi jijini Arusha.
Aliyemshikia zawadi hiyo ni Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga na Afisa
Miradi wa DSW Tanzania Bi. Diana Shuma
(mwenye shati jeupe).
|
 |
Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya
Ujerumani Bibi. Daniela Schadt (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa Shirika la DSW Tanzania wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa
mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini Arusha.Waliokaa kutoka kushoto ni Mke wa
Balozi wa Ujerumani hapa nchini Bibi. Wenday Marshall – Kochanke, Mkuu wa
Wialaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe Munasa, Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter
Owaga na Mratibu wa Programu za Vijana kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Dkt. Elizabeth Mapella. | | |
Habari/Picha: Na Mwandishi Wetu, Arusha
Mke
wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniella Schadt ametoa wito
kwa jamii kuhakiksha wanatoa kipaumbele katika kushirikisha vijana kwenye
nyanja mbalimbali za maendeleo.
Wito
huo umetolewa juzi jijini Arusha wakati Mke huyo wa Rais wa Ujerumani alipokuwa
akizindua mradi wa utetezi na ushawishi wa jamii katika kutoa vipaumbele katika
sekta za Elimu, Afya na Ajira kwa vijana ujulikanao kama BEYOND 2015 ambapo
mradi huo unaratibiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la DSW Tanzania.
Bibi.
Daniela alisema kuwa jamii inapaswa kutoa mkazo katika sekta za Elimu, Afya na
Ajira kwa vijana kwa kuwa duniani kote vijana ndiyo nguvu kazi katika kuletea
maendeleo ya taifa lolote lile.
‘Tunapaswa
kuweka mkazo kwa vijana wadogo, maisha yao ya baadaye yanaanza kuanzia sasa,
tuweke mkazo katika Elimu na Afya kwa vijana wetu ili waeze kutambua fursa na
kuzitumia.’’ Alisema Bibi. Daniela.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bwana Peter Owaga amesema kuwa ni wao
kama asasi ya kirai wanashirikia na Serikali katika kuhakikisha utekelezaji wa
sera zinazohusu vijana nchini zinaleta tija
Owaga
ameongeza kuwa Serikali kama msimamizi imepiga hatu kubwa kwa kuwa na Sera na
miongozo mbalimbali inayohusu vijana kama vile Sera ya Maendeleo ya Vijana ya
mwaka 2007 inayotoa fursa kwa kijana kujitambua.
Aidha
Owaga aliongeza kuwa mradi wa BEYOND 2015 ambao umezinduliwa na Mke wa Rais wa
UjerumaniBibi. Daniela Schadt umelenga kuongeza ushawishi na hamasa kwa
washirika wa maendeleo ili kutoka kipaumbele kwa kutenga bajeti kwa ajili ya
Elimu , Afya ya Uzazi na Ajira kwa vijana.
Akizungumzia
mikakati na namna mradi huo utakavyotekelezwa Afisa Muhamasishaji na
Mawasiliano Bi. Ester Mwanjesa amesema kuwa mradi huo utatekelezwa kwa mwaka
mmoja katika mikoa yote nchini ambapo mijadala mbalimbali itakuwa ikifanyika
ili kuongeza hamasa ya uashawishi utakaopelekea kutoa kipaumbele kwa vijana
hususan katika nyanja za Elimu, Afya ya uzazi na Ajira.
Mradi
huu wa BEYOND 2015 ambao ni kifupi cha maneno Building Expert Youth and Organisation for National Postion on the Post
2015 Development umelenga kutatua changamoto za vijana asa baada ya
kumalizika kwa muda wa Malengo ya Melenia mapema mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni