Jumanne, 16 Desemba 2014

Hatimaye Mtani Jembe kapatikana

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kutoka kulia) akiingia katika katika uwanja wa  Taifa tayari kwa kukagua Timu wakati wa mchezo wa Nani Mtani Jembe baina ya Simba na Yanga uliochezwa siku ya Jumamosi ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2 – 0. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Mecky Sadick, na wapili kutoka kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Jamal Malinzi.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akisalimiana na Kocha Mkuu wa Simba alipokuwa akisalimiana na Benchi la ufundi la timu hiyo alipokuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe baina ya Simba na Yanga uliochezwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na iliibuka na ushindi wa mabao 2 – 0.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akisalimiana na na baadhi ya benchi la ufundi la Timu ya Yanga katika mchezo wa Nani Mtani Jembe baina ya Simba na Yanga uliochezwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na iliibuka na ushindi wa mabao 2 – 0.
Mashabiki wa timu ya Yanga wakifanyavurugu zilizotokana na kuchukizwa na mmoja wa mashabiki kutumia Kitamba chenye rangi nyekundu akiwa katika jukwaa linalotumiwa na mashabiki hao wakati wa mechi ya Nani Mtani Jembe ambapo timu hiyo ililala kwa kufungwa magoli mawili kwa sifuri dhidi ya wapinzani wao Simba S.C.
Screen kubwa iliyopo uwanja wa Taifa ikionyesha matokeo ya mechi ya Nani Mtani Jembe.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kutoka kulia) na Nahodha wa Timu ya Simba Emmanuel Okwi wakiwa wamebeba Kombe la Mshindi wa Kwanza katika mchezo wa Nani Mtani Jembe Timu wakati wa mchezo wa Nani Mtani Jembe baina ya Simba na Yanga mechi iliyochezwa siku ya Jumamosi ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2 – 0.
Mashabiki wa Simba wakifurahia ushindi wao baada ya mechi ya Nani Mtani Jembe kumalizika.

Na Mpiga Picha Wetu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Kumbukumbu la Blogu