Hayo yamesemwa na Meneja wa Kituo cha Huduma kwa
Kanda ya Ziwa (POSO) ambayo ni moja ya
bidhaa ya Godtec, Bwana Emmanuel Kisamba wakati wa Maonyesho ya Wiki yaVijana yanayofanyika
kitaifa mkoaniTabora.
Kisamba aliongezakuwa kupitia huduma hiyo Vijana
wameunganishwa na kutengeneza Kampuni ya huduma za kifedha ya Bega kwa Bega
Microfinace Limted ambayo inamilikiwa na vijana wenyewe na kupitia Kampuni hiyo
vijana wanapata fursa kukopeshwa mitaji kwa ajili ya shughuli zaujasiriamali.
Amezitaja kampuni zilizoanzishwa chini ya utaratibu
huo kuwa ni pamoja na Consultancy in Africa (COAFRI) na Power in Africa (PAFRI),Agri-Business,
Active
Sales and Marketing zenye makao yake jijini Mwanza.
Amesema kuwa majukumu ya kamapuni hizo ni
kuwaelimisha vijana ili wajitambue na kutambua fursa zilizowazunguka nakuzitumia
ipasavyo, kuwawezesha vijana kufungua makampuni yao na kuwashauri vijana katika
miradi wanayotaka kuanzisha. Mengine ni pamoja kuwasadia vijana katika kuandika
maadiko ya miradi endelevu nakutoa ushauri jinsi ya kufanya biashara endelevu
kwa sasa na kwa ajili ya vizazi vijavyo.
“Tunatoa mikopo kwa makampuni ya vijana na kwa
kijana mmoja mmoja”, amesema Bwana Kisamba. Katika mikopo hiyo, dhamana ni hisa
za kampuni inayotaka kukopa. Amefafanua kuwa kila kampuni inabidi inunue hisa
kwenye Bega kwa Bega Microfinance Company Limited ambayo itafanya kampuni
lengwa kupata faida zinazotokana na Bega kwa Bega ikiwemo na kukopesheka.
Meneja huyo alisema kuwa zipo aina tatu za mikopo
ambazo alizitaja kuwa ni Anzisha, mkopo unofikia hadi shilingi milioni 5, Imarisha,
unaofikia milioni 10 na Wekeza ambao kima cha juu ni milioni 50. Mikopo hii
yote ina riba nafuu sana,wastani wa asilimia 10 kwa mwaka, ikilinganishwa na
taasisi nyingine za kifedha nchini.
Hadi sasa jumla ya makampuni manne yameshakopeshwa
na Bega kwa Bega. Meneja Emmanuel Kisamba aliyataja makampuni hayo kuwa ni
COAFRI, PAFRI, Active Sales and Marketing pamoja na Agri-business. Yote haya
yamekopeshwa jumla ya shilingi milioni 22
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa COAFRI Bw.
Ghai Edward vijana watimie fursa inayopatikana kupitia Godtec na washirika wake
kwani na kubainisha kuwa ujasiri na utayari wake baada ya kupata elimu kutoka
kwa maafisa wa Godtec ameweza kuanzisha kampuni yake na kuajiri watu wengi
hivyo amewataka vijana wasibweteke badala yake wathubutu kwa kuanzisha
makampuni.
Ghai ameongeza kuwa kwa kijana akithubutu kujiari
atakuwa amepunguza tatizo la ajira kwake mwenyewe lakini pia atakuwa amewezesha
kuongeza ajira kwa vijana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni