Na: Mwandishi Wetu
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka
watanzania kuendelea kuishi kwa amani na upendo na Wakenya sanjari na kuwa
watulivu wakati wakilifuatilia suala hilo kidiplomasia.
Kauli ya Waziri mkuu,
imekuja kufuatia matamshi ya kibaguzi iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Starehe
nchini Kenya Charles Njagua maarufu kwa jina la kisanii Jaguar ambaye kupitia
kipande chake cha video alisema "Watanzania na Waganda wanaofanya biashara
Kenya, hatuwataki,tunawapa masaa 24 waondoke, wasipoondoka tutawapiga na
hatuogopi mtu."
Hata hivyo kupitia
ukurasa wake wa Twitter, Jaguar amesema kauli aliyoitoa haikumaanisha wakazi wa
ukanda bali aliwalenga Wachina ambao wamevamia biashara zao, kauli inayokinzana
na kilichopo katika viedo yake.
Awali Spika wa Bunge,
Job Ndugai aliwataka wabunge kutoa maoni yao kuhusu kauli hiyo ya kichochezi na
kibaguzi na kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wabunge akiwemo Mwenyekiti wa
Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe.
Wabunge hao wengi wao
waliitaka serikali kutokaa kimya na kuiagiza serikali kulifuatilia suala hilo
kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki suala ambalo
limeshachukuliwa hatua sanjari na wengine kudai siyo la kulipuuza bali ni la
kuitaka Serikali ya KENYA kuomba radhi na kukanusha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni