|
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz alipowasili
kuzindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni,
Kigamboni, jijini Dar es Salam leo Juni 25, 2019.
|
Na: Mwandishi Wetu-MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wafanyabiashara na wauzaji wa
gesi nchini kuuza bidhaa ya gesi tu na
sio mitungi.
Akizungumza katika
hafla ya uzinduzi wa ghala la mitambo ya kuchakata gesi iliyoko Dar-es-salaam, Wilayani
ya Kigamboni, Rais Magufuli amesema kuwa sekta binafsi ni muhimu katika ukuaji
wa uchumi nchini na kuwahakikishia kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana nao.
“Nimefurahi kuona Taifa
Ges mmeanza kukarabati na kutengeneza mitungi yenu wenyewe hii itashusha bei ya
mitungi na kuwawezesha wananchi wengi kutumia gesi, tena kwa hii ikiwezekana
fanyeni kama makampuni ya soda na bia’’, Alisema Rais Magufuli.
|
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa na Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz
kuangalia Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo kabla ya kuvizindua
huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es Salam leo Juni 25, 2019.
|
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati
wa uzinduzi wa Ghala na Mitambo ya kuchakata Gesi ya LPG vya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania huko Vijibweni, Kigamboni,
jijini Dar es Salam leo Juni 25, 2019.
|
|
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa
Ghala na Mitambo ya kuchakata Gesi ya LPG vya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania huko Vijibweni, Kigamboni,
jijini Dar es Salam leo Juni 25, 2019.
Akisisitiza jambo
hili Rais Magufuli ametoa mfano wa Kampuni za Soda na Bia ambapo ukinunua soda na bia maana yake
hulipii creti ila unalipia soda hii itasaidia kupunguza bei ya gesi na
kuwafanya wananchi wengi kutumia nishati hii
Rais Magufuli
amewataka wananchi kutumia Nishati ya
gesi ili kupunguza matumizi ya mkaa, uharibifu wa mazingira, kulinda afya na
kupunguza gharama ya maisha, kwani gunia mbili za mkaa ni sawa na 120,000,
lakini ukitumia gesi gharama yake kwa mitungi miwili ni sawa na 94,000 kwa hiyo
wananchi wakitumia gesi wataweza kuokoa shilingi 26,000.
“uwekezaji huu mkubwa uliofanywa na Taifa Gas
Ltd ni uthibitisho, Serikali yetu inaipenda sekta Binafsi na ipo tayari
kushirikiana na ninyi, kwa hiyo Sekta Binafsi endeleeni kujiamini, endelezeni
kazi pamoja, hapa Tanzania ni mahali
salama kwa uwekezaji”, Rais Magufuli.
|
|
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati na
Madini dkt. Medard Kalemani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya
Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz na viongozi wengine wakikata utepe
kuashiria kuzinduliwa kwa Ghala na
Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar
es Salam leo Juni 25, 2019.
|
|
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati Dkt.
Medard Kalemani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania
Limited Bw. Rostam Aziz na viongozi wengine akikata utepe kuashiria kuzinduliwa
kwa Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya
Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
Rais Magufuli alisema
kuwa Tanzania inahitaji wawekezaji muda wote ili kuwekeza katika sekta ya
nishati kama vile kuzalisha umeme utokanao na Makaa ya mawe, Maji, Upepo pamoja
na Jua ili kuwezesha upatikanajiwa umeme wa kutosha na kwa bei nafuu.
“Wawekezaji
tuwahitaji leo, kesho, kesho kutwa na miaka yote, kwa sababu Tanzania ipo miaka
yote, kwa hiyo wawekezaji na ninyi tunawahitaji
kwa sababu tutakusanya kodi na watanzania watapata ajira kama ambavyo Taifa Gas
mmefanya”, Alisisitiza Rais Magufuli.
Rais Magufuli pia
aliwataka wananchi kutumia Nishati ya gesi ili kupunguza matumizi ya mkaa,
uharibifu wa mazingira, kulinda afya na kupunguza gharama ya maisha, kwani
gunia mbili za mkaa ni sawa na 120,000, lakini ukitumia gesi gharama yake kwa
mitungi miwili ni sawa na 94,000 kwa hiyo wananchi wakitumia gesi wataweza
kuokoa shilingi 26,000.
|
|
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni
ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz na viongozi wengine akifunia
pazia kuashiria kuzinduliwa kwa Ghala na
Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar
es salam leo Juni 25, 2019.
|
|
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mikono wananchi kwa
furaga huku akiwa na msichana baada ya kuzindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni
ya Taifa Gas Tanzania Limited huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam
leo Juni 25, 2019.
|
|
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz
baada ya kuzindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko
Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es Salam leo Juni 25, 2019. (Picha na Ikulu)
Naye Waziri wa
Nishati, Dkt.Medard Kalemani alisema kuwa biashara ya gesi sasa imeendelea
kukua nchini tofauti na hapo zamani ambapo kwa sasa gesi inafika hadi vijijini.
“Biashara hii ya gesi
imekwenda hadi kwenye baadhi ya mikoa, naipongeza na kuishukuru kampuni ya
Taifa ya gesi, ambayo kwa afrika ina maghala makubwa na kuhifadhi na kupokea
gesi kwa Afrika Mashariki na Kusini mwa
Afrika, kwani wanahifadhi tani 7,650, wakifuatiwa na Afrika ya Kusini tani
5,200 huku Morocco wakihifadhi tani 5,077 kwa hiyo sisi ni namba moja”, Alisema
Dkt.Kalemani.
Aidha Dkt.Kalemani
aliongeza kuwa kwa sasa bei ya gesi imeshuka kuliko nchi zote Afrika Mashariki,
kwani kilo moja ya gesi inauzwa Shilingi 3,080, kenya 3,500 huku Uganda ikiuzwa
kwa 4,001.
Dkt.Kalemani alisema
kuwa Sekta ya gesi imepunguza changamoto ya ajira kwa kuajiri wafanyakazi zaidi
ya 12,000 katika kampuni za gesi zilizowekeza nchini.
Biashara ya gesi
nchini ilianza mwaka 1965, huku kampuni ya gesi ya Tipper ilikuwa mshiriki mkuu
wa biashara hiyo, ambapo gesi ilikuwa inatumika viwandani, Mashuleni, katika
Taasisi za Serikali na Vyuoni.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni