Na:
Frank Shija
Wafanyabiashara
ndogondogo katika Soko la Machinga Complex Jijini Dar es Salaam wameshauriwa
kubadilika na kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia sheria badala ya kufanya
biashara zao kimazoea.
Wito
huo umetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene alipofanyaa ziara ya kikazi katika Soko
hilo ili kusikiliza changamoto wanazokumbana nazo wafanyabiashara wa soko hilo.
“Nawapa
pole sana ndugu zangu wafanyabiashara wa Machinga Complex mnaendesha biashara
zenu bila kuzingatia sheria jambo linalo wagharimu hivi sasa katika biashara
zenu leo nimekuja kuwarejesha kwenye mstari,” alisema Simbachawene.
Aidha
Waziri Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuwachukulia
hatua baadhi ya viongozi wa menejimenti ya Machinga Complex kwa kile
kinachodaiwa utendaji wao mbovu na kujaza nadfasi zote zilizo wazi,
Wakati
huohuo amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuteua Wajumbe wa
Bodi ya Machinga Complex ili kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa Soko hilo.
Pia
Waziri Simbachawene ametoa wito kwa wafanyabiashara wote kulipa kodi zao kwa
wakati huku hakitishia kuwaondoa katika vizimba (eneo la mraba la mauzo) wale wote
watakao kaidi amri hiyo halali ya kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na mikataba
yao.
Awali
akimkaribisha Waziri Simbachawene, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
amesema kuwa ujio wa Waziri huyo mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa imekuja
wakati muafaka kwani ni takribani kipindi cha karibu mwaka mmoja tangu alipompa
maagizo ya kushughulikia changamoto zinazokabili jengo la Machinga Complex kazi
ambayo waliikamilisha na kukabidhi taarifa katika ofisi ya Waziri Simbachawene.
“Nidhahiri
kuwa ziara yako Mhe. Waziri itatoa majawabu yatakayopelekea kutatua changamoto
kadhaa zinazolikabili soko hili la Machinga Complex na ni imani yangu kwamba
utatoa maagizo na kufanya maamuzi nasi hatuna budi ya kuyapokea na kutekeleza”
alisisitiza Makonda.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bibi. Sipora Liana amesema kuwa
changamoto kubwa inayokabili Soko hilo ni pamoja na deni linalokadiriwa kufikia
zaidi ya shilingi bilioni 38 zianzodaiwa na Shirika la hifsdhi za Jamii (NSSF)
ambao ndiyo waliojengwa majengo ya soko hilo linalomilikiwa na Halmashauri ya
Jiji la Dar es Salaam.
Aliongeza
kuwa changamoto nyingine inayokabili Soko hilo ni kutokuwapo kwa chombo cha
maamuzi (Bodi) ambayo kazi yake kubwa ingekuwa kushughulikia changamoto zote za
mradi huo.
Soko
la Machinga Complex limejengwa kwa lengo la kutatua changamoto ya ukosekanaji
wa soko la uhakika kwa wafanyabiashara wadogowadogo katika Jiji la Dar es
Salaam ambapo ujenzi wake ulifanyika chini ya udhamini wa NSSF na kumilikiwa na
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam likiwa na uwezo wa kuchukua takribani
wafanyabiashara 4206.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni