ta
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James
Wambura(kulia) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi.Nuru Millao(katikati) alipowasilia
katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo Jijini Dar es Salaam tayari kwa
kufungua Warsha ya Kamati ya Urasimishaji kuhusu sekta ya Ubunifu iliyoandaliwa
na Bodi ya Filamu Tanzania,kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo.
 |
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James
Wambura(kulia) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo Bibi.Nuru
Millao(kushoto) alipowasilia katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo tayari
kwa kufungua Warsha ya Kamati ya Urasimishaji wa sekta ya Ubunifu iliyoandaliwa
na Bodi ya Filamu Tanzania.
|
 |
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michszo Bibi.Nuru Millao(kushoto) akiongea kabla ya
kumaribisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Anastazia Wambura (katikati) wakati
wa ufunguzi wa warsha ya Kamati ya Urasimishaji kuhusu sekta ya Ubunifu
iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya
Filamu Tanzania Bibi.Joyce Fissoo.
|
 |
| Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Anastazia James Wambura(katikati) akiongea na wajumbe wa Kamati ya
Urasimishaji kuhusu sekta ya ubunifu wakati wa ufunguzi wa warsha ya wajumbe hao
leo Jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo Bibi.Nuru Millao na kushoto kwake ni
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.Joyce Fissoo. |
 |
.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma ya Ufundi kutoka Bodi ya Filamu Tanzania
Bw.Romanus Tairo akiwasilisha mada kuhusu
sekta ya ubunifu wakati wa warsha ya kamati ya urasimishaji ya sekta
hiyo leo jijini Dar es Salaam.
|
 |
Mkufunzi
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.Mona Mwakalinga(kushoto) akifafanua
jambo alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu
uwezo wa sekta ya filamu katika kuchangia uchumi katika warsha ya kamati
ya urasimishaji wa sekta ya ubunifu leo Jijini Dar es Salaam,kulia ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Hakimiliki na Shiriki Tanzania (COSOTA).
|
 |
Mkurugenzi
Msaidizi Tathmini na Ufuatiliaji Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Bernard
Lubobo akiuliza swali katika warsha ya
kamati ya Urasimishaji kuhusu sekta ya Ubunifu iliyofanyika leo Jijini Dar es
Salaam.
|
 |
Kaimu
Mkurugenzi Kitengo cha Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Bibi.Leah Kihimbi akichangia hoja katika warsha ya Kamati ya Urasimishaji
kuhusu sekta ya ubunifu leo Jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Bodi ya
Filamu Tanzania ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa.
|
 |
Wajumbe
wa Kamati ya Urasimishaji kuhusu sekta ya Ubunifu wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwasilishwa na wawezeshaji leo Jijini Dar es Salaam.
|
 |
Wajumbe
wa Kamati ya Urasimishaji kuhusu sekta ya Ubunifu wakiimba wimbo wa kuhamasisha
ushirikiano katika warsha iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania ambapo mada
mbalimbali ziliwasilishwa na wawezeshaji leo Jijini Dar es Salaam.
Picha/Habari Na
Lorietha Laurence
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura
ameitaka kamati ya urasimishaji sekta za ubunifu kuweka mfumo rasmi wa
kuwatambua wadau wa sekta hizo ili waweze kuwasimamia.
Mhe.
Anastazia ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua warsha
iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania ambapo alieleza kuwa kwa kuwepo kwa
mfumo rasmi wa kutambaua sekta hizo
kutarahisisha kuwatambua wasanii katika makundi mbalimbali.
“Sekta
ya ubunifu ni pana na muhimu katika kukuza pato la mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla
hivyo ni muhimu kurasimisha kwa kuwepo mfumo rasmi wa kuitambua” amesema Mhe.
Anastazia.
Anaongeza
kuwa kwa kutambua umuhimu wa sekta ya ubunifu Rais wa awamu ya tano Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli aliamua kufuata ilani ya chama cha Mapinduzi katika kuunda
Wizara ambayo inajihusisha na mambo ya sanaa.
Naye
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru
Millao amesema kufuatia warsha hiyo anaamini itasaidia kamati ya urasimishaji
kujipanga katika kusimamia kazi za filamu na muziki ili kuwa ajira rasmi yenye
kuingizia watu kipato.
“Mbali
ya sekta hii ya ubunifu kuwa rasmi pia
itasaidia katika kusambaza elimu kwa umma kuhusu mchango unaofanywa na sekta hiyo
katika kukuza uchumi na kuongeza ajira nchini” alisema Bibi. Nuru.
Aidha
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo ameeleza kuwa
warsha hiyo ipo katika kuwajengea uwezo wanakamati katika kuimarisha uelewa na
kuifanya sekta ya ubunifu kuwa rasmi.
Kwa
upande wake Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Mona Mwakalinga
amefurahishwa kuona Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inathamini
mchango wa kazi zote za ubunifu kwa kutaka kuzirasimisha kwani kwa kufanya hivyo
itasaidia kuinua kazi za ubunifu na kuzifanya kutumika zaidi nje ya nchi.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni