Jumapili, 3 Julai 2016

TECNO YAFANYA PROMOSHENI KUBWA WASHINDI 100 WAPATIKANA.




Kampuni maarufu ya Simu Tecno Mobile imefanya promosheni kubwa inayohusiana na simu yao mpya inayokuja nchini hivi karibuni TECNO CAMON  C9 katika eneo la City Mall, Kisutu jijini Dar es Salaam.

Simu janja (smartphone) ya TECNO CAMON C9 ndiyo simu yenye kamera bora zaidi inayokuja katika soko kwa sasa hivyo katika promosheni hiyo Zawadi mbalimbali zimetolewa kwa washindi 100 ambao waliweza kuagiza simu hiyo mapema kuanzia 21 mwezi wa sita mpka  2 mwezi wa saba kwa kiasi cha shilingi elfu thelathini (30,000) ambayo itamaliziwa simu ikifika kwa mtumiaji.

Akizungumza wakati wa promosheni hiyo meneja wa mauzo wa TECNO Mobile Tanzania, Bw.Fred Kadinala amesema kua TECNO inawajali watumiaji wa simu zake hivyo kuamua kuwapa zawadi kubwa na kuwaruhusu waagize simu kwa bei ndogo ili wapate simu hiyo mapema Zaidi.

Zawadi kubwa kama TV screen yenye wa inchi 42 imetolewa kwa mshindi wa kwanza yenye thamani ya million moja na nusu, washindi wengine akijishindia Carlcare VIP card yenye thamani ya shilingi laki 3(300,000)  itakayomuwezesha kutengenezewa simu yake  bure mwaka mzima kwa tatizo lolote litakalotokea na pia kifurushi maalumu cha zawadi kutoka kampuni ya Tecno.

Promosheni hiyo iliyoanza saa nane mchana kwa michezo mbalimbali iliyowavutiwa watazamaji wengi baada ya hapo washindi Zaidi ya mia moja waliojishindia zawadi mbalimbali ikiwemo rice-cooker, jagi la umeme, oven, na vifurushi vya zawadi kemkem tokea kampuni ya Tecno Mobile Tanzania.

Simu ya TECNO CAMON C9 inatajiwa kuingia sokoni rasmi kuanzia mwezi wa saba nchini Tanzania tayari kwa mtu yoyote kuinunua na kufurahia uzuri wa kamera yake.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Kumbukumbu la Blogu