|
MAHAKAMANI KWA KUPOKEA
RUSHWA YA DOLA 3,000
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Kinondoni imemfikisha mahakamani Afisa
wa Uhamiaji wa Manispaa ya Kinondoni Bi. Margreth Kokushubira Prosper mnamo
tarehe 1/2/2016 kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15(1)(a)
cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2007. Kesi hiyo
Na. 01/2016 iko mbele ya Mhe. Hakimu Obadia Bwegoge.
Bi.
Margreth mwenye umri wa miaka 33, alikamatwa tarehe 27/1/2016 katika eneo la
kuegesha magari lililopo nje ya jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa
kupokea rushwa ya fedha za kimarekani dola 3,000 kutoka kwa raia wa China Bw. Lizhi
Ping. Bi. Margret alikuwa ameomba hongo hiyo kwa raia huyo wa China apate
kumrudishia hati kumi za kusafiria za raia wenzake zilizokuwa zikishikiliwa na
ofisi ya Uhamiaji ya Wilaya ya Kinondoni. Hati hizo zilikuwa zinashikiliwa na
ofisi hiyo kwa ajili ya kuzikagua kufuatia agizo lililotolewa na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Jenister Mhagama la kuwatambua na kuwakamata raia wa kigeni
wanaoishi na kufanya kazi nchini bila kuwa na vibali. Hivi sasa mshtakiwa yuko
nje kwa dhamanana kesi yake itatajwa tena tarehe 24/2/2016.
Dola
hizo 3,000 alizokamatwa nazo ni sehemu ya dola 6,000 alizokuwa ameomba sawa na
fedha za kitanzania shilingi milioni kumi na tatu (13,000,000/-) kutoka kwa Bw.
Lizhi Ping.
Mkuu
wa TAKUKURU (M) Kinondoni Bw. Benn Lincolin anatoa onyo kwa watumishi wa umma
wenye tabia kama ya Bi. Magret Kokushubira Prosper ya kujinufaisha kutokana na
maagizo yanayotolewa na viongozi wa Serikali, kuacha tabia hiyo vinginevyo
sheria itachukua mkondo wake.
IMETOLEWA
NA MKUU WA TAKUKURU (M) KINONDONI
BENN
LINCOLIN
2/2/2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni