Wafanyakaz wa umati wakiwa na watoto yatima pamoja
na walezi wa watoto yatima katika kituo cha watoto yatima Kurasini
Chama cha uzazi na malezi bora(UMATI) kupitia
kituo chake cha vijana umati temeke walitembelea kituo cha watoto yatima
kurasini tarehe 17.1.2015 ili kutoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa
vijana hao ili kuwasaidia kuepuka vishawishi vya ngono na makundi rika ambayo
si mazuri na yatakayoharibu mwenendo wao wa maisha ya baadae na afya zao
kiujumla. Athari hizo ni kama mimba katika umri mdogo,kupata maambukizi ya
ukimwi na magonjwa mengine ya ngono,kutumia vilevi na madawa ya kulevya n.k
Picha kwa Hisani ya Kituo cha Vijana,UMATI-TEMEKE
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni