Timu
ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waaswa kuwa mfano katika
mashindano ya SHIMIWI ikizingatiwa kuwa ipo chini ya Wizara inayo simamia
michezo nchini.
Wito
huo umetolewa leo jiji Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi Sihaba Nkinga wakati Timu hiyo ikiagwa rasmi
kwa ajili ya kuelekea Mkoani Morogoro kwa kushiriki mashindano ya SHIMIWI 2014
yanayotarajiwa kuanza tarehe 27 Septemba hadi
tarehe 11 Oktoba.
Bibi
Sihaba pia amewataka wanamichezo hao kuwa
na nidhamu katika michezo, kuzingatia sheria na kanuni zinazoongoza
michezo watakayoshiriki na kujituma kwa
lengo la kuleta ushindi.
“Kumbukeni
kuwa ninyi ni Watumishi wa Umma hivyo mnapaswa kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma katika kutelekeza
dhamira ya mashindano hayo”.Amesema Bibi Nkinga.
Kwa
upande mwingine Bibi Sihaba amewashukuru wadhamini mbalimbali wakiwemo Platinum
Credit Ltd,Starmedia (Startimes)TFF,WaterCom (T) Ltd na Mohamed Enterprise kwa kushirikiana na Wizara kuinua michezo kwa
kuchangia vifaa mbalimbali vya michezo ili kufanikisha mashindano hayo.
Naye
Mwenyekiti wa Timu Dkt. Margret Mtaki ameushukuru uongozi wa Wizara kwa kuwapa ushirikiano mzuri
katika kufanikisha maandalizi ya Timu kwa
kuwapatia vifaa vya kutosha katika michezo yote.
Pia
Mwenyekiti ameahidi kuwa Timu itazingatia nidhamu ya hali ya juu na kujituma ili kuelete
ushindi wa kishindo kwa Wizara.
Aidha,
Mshindi wa Mchezo wa Drafti na Kurusha Tufe katika Mashindano ya SHIMIWI 2013
na Mashindano ya Mei Mosi 2014 Bi. Niuka
Chande amekabidhiwa zawadi ya sh.
300,000 na cheti cha kutambua mchango wake katika michezo hiyo na kuiletea Wizara ushindi.
Timu
ya Wizara mwaka huu inajumuisha jumla wachezaji 55 amabao watashiriki michezo
mbalimbali ikiwemo Mpira wa
Miguu,Riadha,Mpira wa Pete,Drafti,Karata, Bao na Kuvuta Kamba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni