Frank
Mvungi-Maelezo
Serikali
imewataka wananchi kujihadhari na makampuni yanayojiingiza katika kazi za
upimaji ardhi au uthamini bila ya kusajiliwa na bodi au Halmashauri zenye mamlaka ya
kusimamia taaluma husika.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara
ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi bw.Justo Lyamuya wakati wa mkutano na
waandishi wa habari uliolenga kutoa utaratibu unaotakiwa kufuatwa na wananchi
katika upimaji ardhi.
“Hadi
sasa wapima ardhi waliosajiliwa ni 290 wakati makampuni yaliyosajiliwa na
Baraza la Taifa la wapima na wathamini ardhi ni 58” hivyo hakuna haja ya
wananchi kutapeliwa na vishoka. Alisema Bw. Lyamuya.
Akifafanua
Lyamuya amesema kuwa ni vyema wananchi wakatumia makampuni yaliyosajiliwa
kufanya kazi ya kupima ardhi ili kuepuka migogoro ambayo kwa kiasi kikubwa
inachangiwa na ukiukwakwaji wa sheria na taratibu za upimaji ardhi.
Akifafanua
kuhusu wathamini (valuers) Lyamuya amesema hadi sasa wataalamu waliosajiliwa ni
320 na makampuni yalisajiliwa na Baraza ni 54.
Pia
Lyamuya alisema kuwa kazi za upimaji viwanja zitakazowasilishwa Wizarani ambazo
hazikufuata taratibu na kwa mujibu wa sheria ya upimaji Ardhi sura 324 ya mwaka
1957 hazitapokelewa.
Pia
mambo yanayopaswa kuzingatiwa katika upimaji wa ardhi (mashamba na viwanja)
lyamuya amesema upimaji usiozingatia ushirikishwaji na kutambua mipaka kwa
maridhiano hautapokelewa.
Aidha
makampuni ya upimaji yanayowasilisha kazi za upimaji kwa Mkurugenzi waUpimaji
na Ramani ambazo hawakuzisimamia wao wenyewe au wawakilishi wao na
kudhibitika;kazi hizo hazitapokelewa na kwa mujibu wa sheria za kusajili
makampuni ya upimaji Na.2 ya mwaka 1977 yataadhibiwa ikiwa ni pamoja na
kusimamishwa.
Halmashuri
ya Taifa ya wapima Ardhi ni chombo cha Serikali kilichoundwa kwa mujibu wa
sheria Na.2 ya mwaka 1977,Jukumu kubwa la chombo hiki ni kufanya usajili wa
wataalam wapima Ardhi,kusimamia weledi wa taaluma na mwenendo wa utendaji
katika masuala ya kupima ardhi (Land Survey) kuthamini mali (property
valuation) na kuendeleza ardhi (estate management).


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni