![]() | |||
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi akitangaza uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya
Kongwa Deogratius John Ndejembi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
IKULU
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016
amemteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani
Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi amesema Bw. Deogratius John Ndejembi anachukua nafasi
iliyoachwa na aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. John Ernest
Palingo ambaye amehamishiwa Wilaya ya Mbozi katika Mkoa wa Songwe.
Uhamisho wa Bw. John
Ernest Palingo kwenda Wilaya ya Mbozi, umefanywa baada ya Mhe. Rais Magufuli
kuridhia maombi ya Bw. Ally Masoud Maswanya aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Mbozi, kuomba uteuzi wake utenguliwe kutokana na sababu binafsi.
Bw. Deogratius John
Ndejembi atakula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma siku ya
Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi
wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
07 Julai, 2016
|
Alhamisi, 7 Julai 2016
Rais Dkt. John Pombe Magufuli afanya Uteuzi wa Wakurugenzi wa Majiji Matano (5) Manispaa 21, Miji 22, Na Halamashauri za Wilaya 137.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni