 |
Mwenyekiti wa Jukwaa la
Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF) Bw. Erick Chrispin akizungumza wakati wa
mkutano wa Jukwaa hilo unaofanyika kila mwisho wa mwezi jana jijini Dar es
Salaam. Mada kuu katika mjadala huo ilikuwa ni “Jinsi gani Asasi zinawezakutumia
Ujasiriamali wa Kijamii katika kuibua na kuhakikisha inafikia malengo yake”
|
 |
Afisa Mtendaji Mkuu wa
Asasi ya Open Mind Tanzania (OMT) ambaye pia ni Mratibu wa Programu ya Kukuza
Ajira zenye staha jijini Dar es Salaam(YEID) Bw. Dominic Ndunguru akiwasilisha
maada kuhusu misingi ya ujasiriamali wakati wa mjadala kuhusu “Jinsi gani Asasi zinawezakutumia Ujasiriamali
wa Kijamii katika kuibua na kuhakikisha inafikia malengo yake” jana jijini Dar
es Salaam. Mjadala huo uliratibiwa na
Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF).
|
 |
Meneja Matukio na
Ushirikiano wa Asasi ya Buni Innovation Hub Bi. Maryam Mgonja akielezea kuhusu
namna asasi yao inavyofanya kazi wakati wa mjadala kuhusu “Jinsi gani Asasi
zinawezakutumia Ujasiriamali wa Kijamii katika kuibua na kuhakikisha inafikia
malengo yake” jana jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliratibiwa na Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania
(TASEF).
|
 |
Afisa Mtendaji Mkuu wa Sema
Tanzania Bw. Kiiya Joel Kiiya akifafanua jambo wakati wa mjadala kuhusu “Jinsi
gani Asasi zinawezakutumia Ujasiriamali wa Kijamii katika kuibua na kuhakikisha
inafikia malengo yake” jana jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliratibiwa
na Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania
(TASEF)
|
 |
Mmoja wa washiriki wa
Mjadala kuhusu “Jinsi gani Asasi zinawezakutumia Ujasiriamali wa Kijamii katika
kuibua na kuhakikisha inafikia malengo yake” ambayepia ni mwanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Bi. Liliani Kimaro akiwasilisha hoja
walizozipata wakati wa majadiliana kwenye kundi lao jana jijini Dar es Salaam.
Mjadala huo uliratibiwa na Jukwaa la
Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF).
|
 |
Mmoja wa washiriki wa
Mjadala kuhusu “Jinsi gani Asasi zinawezakutumia Ujasiriamali wa Kijamii katika
kuibua na kuhakikisha inafikia malengo yake akichangia mada wakati wa
majadiliano jana jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliratibiwa na Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania
(TASEF).
|
 |
Baadhi ya washiriki wa
Mjadala kuhusu “Jinsi gani Asasi zinawezakutumia Ujasiriamali wa Kijamii katika
kuibua na kuhakikisha inafikia malengo yake” wakifuatilia mada wakati wa
majadiliano jana jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliratibiwa na Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania
(TASEF).
|
 |
Mmoja wa washiriki wa
Mjadala kuhusu “Jinsi gani Asasi zinawezakutumia Ujasiriamali wa Kijamii katika
kuibua na kuhakikisha inafikia malengo yake”. Akifafanua namna ujasiriamali
unavyo tegemea zaidi kuanza na wazo badala ya mtaji jana jijini Dar es Salaam.
Mjadala huo uliratibiwa na Jukwaa la
Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF).
Picha/Habari na: Frank Shija
|
Watanzania
hasa vijana wameaswa kutumia mbinu za Ujasiriamali Jamii katika kukabiliana na
changamoto za kimaendeleo miongoni mwa jamii zinazowazunguka.
Rai
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF)
Bw. Erick Chrispin wakati wa mjadala kuhusu Jinsi gani Asasi zinaweza kutumia
Ujasiriamali wa Kijamii katika kuibua na kuhakikisha inafikia malengo yake”
uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Chrispin
amesema kuwa ilikutatua changamoto na matatizo ya kijamii vijana wanawajibu wa
kufikiri namna ya kutumia changamaoto hizo kama njia mbadala ya kujipatia
kipato kwani kufanya hivyo kunafaida kwa pande zote.
“Ujasiriamali
Jamii ndiyo suluhu tena endelevu katika kukabiliana na changamoto za
kimaendeleo katika jamii zetu,chukulia mfano kuna tatizo la maji, unachimba
kisima unauza maji kwa gharama nafuu, jamii inapata maji hali kadharika na wewe
unaingiza kipato.Huo ndiyo Ujasiriamali ninaoungelea.” Alisema Chrispin
Aidha
aliongeza kuwa kwa kuona umuhimu wa Ujasiriamali Jamii Jukwaa hilo lilianzishwa
ili kusahidia kutoa hamasa kwa vijana nchini waweze kushiriki na kubuni mambo
mbalimbali katika kutekeleza dhana ya Ujasiriamali Jamii.
Alisema
kuwa ni faraja kuwa jamii kwa kiasi kikubwa imeitikia katika kutumia aina hiyo
ya ujasiriamali na hasa inatokana na msukumo wa soko huria na kupungua kwa
wahisani katika kugharamia shuguli za kijamii.
Jukwaa
la Ujasiriamali Jamii Tanzania (Tanzania Social Entrepreneurship Forum
–TASEF) lilianzishwa mwaka 2012 ikiwa ni
kwa njia ya Mtandao na baada ya kupata wadau wengi mnamo mwaka 2015 TASEF
ikazaliwa rasmi na mpaka sasa jumla ya mikutano 9 ya majadiliano katika mada
mbalimbali imekwisha fanyika, mijadala hiyo ufanyika kila mwisho wa mwezi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni