Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu
wanawake “Twiga Stars” wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (hayupo pichani) alipowatembelea kambini
kwao leo jijini Dar es Salaam.Twiga Stars inatarajiwa kucheza mechi na Timu ya
Taifa wanawake ya Zimbabwe mchezo utakaochezwa tarehe 4 katika uwanjja wa
Taifa.
Picha/Habari na: WHUSM
Serikali
kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa motisha kwa
wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake(Twiga Stars) ikishinda
katika mchezo wake dhidi ya Zimbabwe unatarajiwa kuchezwa siku ya Ijumaa tarehe
4 machi katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Haya
yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia
James Wambula alipotembelea kambi ya Timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na wachezaji wa Twiga Stars, Wambura amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na
wadau wa michezo wamekusanya shilingi milioni 15 ambazo zitatumika kama motisha
kwa wachezaji hao.
Naibu
Waziri huyo aliongeza kuwa iwapo timu hiyo itaibuka na ushindi katika mechi
yake dhidi ya Zimbabwe kila mchezaji atapata gawio la sh. Laki tatu kama
mptisha na kuongeza kuwa itafanyika hivyo hivyo katika mchezo wa marudiano
utakaochezwa nchini Zimbabwe.
Aidha
alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa michezo kuzidi kujitokeza na kuisaidi
timu hiyo ikiwa ni pamoja na kuhudhuria kwa wingi katika mechi ya tarehe 4
machi dhidi ya Zimbabwe itakayochezwa katika uwanja wa Taifa.
Aliongeza
kuwa msaada zaidi unahitajika ili kuiwezesha timu hiyo kukidhi mahitaji yake
muhimu,hivyo alitoa wito kwa wadau mbalimbali kutoa michango yao kupitia Twiga
Specila Fund, Akaunti na: 20110001677 iliyoko NMB tawi la Bank House jijjini
Dar es Salaam.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesiga ameipongeza Serikali kwa
jitihada zake za kuhakikisha Twiga Stars inapata huduma muhimu ikiwemo motisha kwa
wachezaji na benchi la ufundi.
Mwesiga
pia amewapongeza wadau wote waliojitolea kusaidi timu hiyo ambapo amesema
kujitokeza kwa wadau hao kunaongeza morali ya wachezaji.
Msaada
huo wa shilingi milioni 15 umetolewa na wadau watatu ambapo mmja aliyechangia
sh. Milioni 3 aliomba jina lake lihifadhiwe, wengine ni Kampuni ya ASAS sh.
Milioni 2 na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) sh. Milioni 10.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni