 |
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye alipowasili katika Uwanja wa Ndani wa Michezo kabla ya
kikao baina yake na wadau na viongozi wa vyama vya michezo jana jijini Dar es Salaam.
|
 |
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akielekeza jambo kuhusu mradi wa
kuendeleza Uwanja wa Ndani wa michezo jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia
ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole
Gabriel na wa mwisho kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick.
|
 |
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akimsikiliza kwa makini Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipowasili katika
Uwanjwa wa Ndani wa Michezo kabla ya kikao baina yake na wadau na viongozi wa
vyama vya michezo jana jijini Dar es Salaam.
|
 |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye akifafanua jambo kabla ya kikao cha wadau wa michezo na Waziri
Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa(hayupo pichani) jana jjijini Dar es Salaam.Kutoka
kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bibi. Sophia Mjema, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Said Meck Sadick, na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Annastazia Wambura.
|
 |
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Annastazia Wambura akifuatilia maelezo kuhusu mradi wa kuendeleza eneo
changamani la michezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw.
Makoye Nkenyenge jana jijini Dar es Salaam.
|
 |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akisalimiana na Rais wa Shirikisho la
Mpira Miguu Tanzania (TFF) Bw. Jamal Malinzi walipokutana katika kikao baina ya
viongozi hao na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa (hayupo pichani) jana
jijini Dar es Salaam.
|
 |
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
Bw.Dioniz Malinzi akizungumza wakati wa kikao cha viongozi wa vyama vya michezo
na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa (hayupo pichani) jana jijini Dar
es Salaam.
|
 |
Mmoja wa viongozi wa vyama vya michezo akichangia
hoja wakati wa kikao baina yao na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa
(hayupo pichani) kilichofanyika katika ukumbi wa Uwanjja wa Taifa jana jijini
Dar es Salaam.
|
 |
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akakifurahia jambo baada ya kumaliza
kikao na wadau na viongozi wa vyama vya michezo jana jijini Dar es Salaam.Kulia
kwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante
Ole Gabriel na wa mwisho kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Zawadi Msalla
|
 |
Waziri Mkuu wa Jjamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Majaliwa Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la
Michezo la Taifa (BMT) mara baada ya kumaliza kikao baina yake na vingozi wa
vyama vya michezo jana jijini Dar es Salaam.Waliokaa kutoka kushoto ni Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura, Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel, Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye,Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la
Taifa BMT Bw. Dioniz Malinzi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick na
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bibi. Sophia Mjema.
|
 |
Waziri Mkuu wa Jjamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Majaliwa Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadhamini wa
michezo nchini mara baada ya kumaliza kikao baina yake na vingozi wa vyama vya
michezo jana jijini Dar es Salaam.Waliokaa kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura, Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye,Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Bw.
Dioniz Malinzi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick na Mkuu wa
Wilaya ya Temeke Bibi. Sophia Mjema.
|
 |
Waziri Mkuu wa Jjamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Majaliwa Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa
vyama vya michezo nchini mara baada ya kumaliza kikao baina yake na vingozi hao
jana jijini Dar es Salaam.Waliokaa kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Profesa Elisante Ole Gabriel, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye,Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Bw. Dioniz
Malinzi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick na Mkuu wa Wilaya ya
Temeke Bibi. Sophia Mjema.
Picha zote na Frank Shija |
Na
Lilian Lundo
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameyataka makampuni na wafanyabiashara
kutangaza biashara zao kupitia uwanja wa Taifa.
Mhe.
Majaliwa aliyasema hayo katika mkutano wa wadau wa michezo wakiwemo wadhamini
wa michezo, vyama vya michezo vya Taifa na mashirikisho uliofanyika katika moja ya kumbi zilizopo
uwanja wa Taifa.
“Uwanja
wetu una hadhi ya kimataifa lakini uwanja huu hautumiki kutangaza biashara
yoyote kama chanzo cha mapato, badala
yake kuta za uwanja zimezungukwa na giza hasa muda cha usiku,” alisema
Mhe. Majaliwa.
Mhe.
Majaliwa aliongeza kwa kusema kuwa kama
uwanja huo utazungukwa na mabango ya matangazo yataupandisha hadhi
na kubadilisha mandhari ya uwanja hasa muda wa usiku na fedha zitakazopatikana zitatumika kuboresha
uwanja huo.
Hivyo
Mhe. Majaliwa amewataka wadhamini wa michezo kujitokeza kwa wingi kutumia fursa
hiyo ya kutangaza bidhaa au huduma wanazozitoa kupitia uwanja wa Taifa ambao
hutumika katika mechi nyingi za kitaifa na kimataifa zinazochezwa nchini.
Aidha,
Mhe. Majaliwa amesema kuwa Tanzania itaendelea kupata heshima kupitia sekta ya
michezo kwani michezo ni kielelezo kinachoweza kutambulisha utamaduni wa Taifa
hivyo wadau wa michezo washikamane na Serikali na kuona ni namna gani matatizo
ya michezo yatatatuliwa na michezo kuendelezwa nchini.
Serikali
ya awamu ya tano imejipanga kuendeleza michezo nchini kwa kuweka misingi imara
ya kuendeleza michezo kuanzia umri wa chini, kurekebisha sera na sheria za
michezo ziliopitwa na wakati, kujali mafanikio, matatizo na mambo muhimu
yanayohusu michezo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni