WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI ,SANAA NA MICHEZO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MTUMISHI
WA WIZARA YA HABARI AFARIKI KWA AJALI YA
GARI.
Kufuatia kifo cha Mfanyakazi
wa Bodi ya Filamu Tanzania Bwana Jovitha
Dellan, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante
Ole Gabriel ameitumia
salamu za Rambirambi familia ya Mzee Dellan Tarmo kufuatia kifo kijana wao
mpendwa kilichotokea juzi (tarehe 31.1.2016)kwa ajali ya gari mkoani Arusha.
“Pokea
rambirambi zangu za dhati, sote kwa pamoja tumepoteza kijana mchapakazi, hodari na aliyependa kushirikiana
na wenzake katika kazi zake, hakika tutamkumbuka siku zote” Katibu Mkuu amesema.
Katibu Mkuu, Pia amemtumia salamu
za pole kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu(KBF) na Wafanyakazi wote wa Bodi
ya Filamu Tanzania.
“Nimepokea
taarifa za kifo cha Jovitha Dellan kwa huzuni kubwa, najua machungu na maumivu
mliyonayo kwa kuondokewa na kiungo muhimu katika utendaji wenu, poleni
sana, niko nanyi katika msiba huu mzito
kwenu”, amesema
Katibu Mkuu huyo.
Katibu Mkuu amesema pamoja na
kwamba kifo hakiepukiki, bado ni kitu ambacho kinashtua, kuhuzunisha na kuleta
unyonge mkubwa kwa wafiwa katika jamii.
“Naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu
kumuombea kijana wetu Jovitha Dellan ili mwenyezi Mungu ampe mapumziko mema ya
Milele” Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape uvumilivu
na subira katika kipindi hiki”.
“Niko
nanyi katika kipindi hiki kigumu kwa hali na mali, nawaomba msijisikie wapweke” Katibu Mkuu amesema na kuwatakia
utulivu na amani katika kipindi hiki cha msiba mkubwa kwa familia.
Marehemu Jovitha Dellan amefariki juzi tarehe 31 Januari, 2016 mkoani
Arusha ambapo alikuwa njiani kurejea kazini jijini Dar es salaam.
Marehemu
Jovitha Dellan anatarajiwa kuzikwa wiki hii mkoani Manyara .
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Jovitha
Dellan mahali Pema Peponi, Amina.
Mwisho
Imetolewa
na:
Idara ya
Habari(MAELEZO)
DSM.
2 Februari, 2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni