![]() |
Picha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Angella Kairuk akijibu maswali toka kwa wabunge katika kikao cha 6 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma. |
(Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO)
Serikali
imejipanga
kuborsha zaidi mpango wa kunusuru Kaya masikini nchi ujulikanao kama
TASAF kwa awamu ya tatu kwa kutengeneza miundombinu mizuri ya kutambua
Kaya zinazolengwa
na kuondoa malalamiko ya wananchi kuwa mpango huu umekuwa ni wa Kaya
chache na fedha
hizo utolewa kwa upendeleo.
Akijibu swali la
Mhe.Magdalena Hamisi Sakaya Mbunge wa Kaliua (CUF) lililouliza ni vigezo gani
vinatumika kuondoa Kaya zilizopendekezwa kwenye mradi na kubakiza Kaya chache,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angella Kairuki amesema mpango wa kunusuru Kaya maskini hutambulishwa
kijijini na wataalam kutoka Halmashauri husika kwa kusimamiwa na uongozi wa
kijiji kisha kuweka vigezo vya Kaya maskini.
“ Wakusanya
taarifa huchaguliwa kutoka miongoni
mwa vijana wanaoishi kijijini hapo na kupitia nyumba kwa nyumba
kuorodhesha Kaya ambazo zinakidhi vigezo vilivyoanishwa na mkutano wa
Kijiji ila bado kuna
malalamiko yanayotolewa kuwa Kaya maskini zinaachwa na kupewa Kaya
nyingine
ambazo sio maskini kwa kuliona tatizo
hilo suala hili tunalifanyia uchunguzi na tunaomba watu watoe taarifa ikiwa wataona ukiukwaji wa uorodheshaji wa Kaya
zitakazohusika na mpango huu ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi ya yoyote
atakaye bainika kufanya hivyo”
“ Mpaka sasa kutokana
malalamiko yaliyojitokeza katika kuorodhesha Kaya maskini zinazotakiwa kuwezeshwa
na mpango huu tumewaajibisha watendaji toka Wilaya za Karagwe, Kagera na Kibondo,
Kigoma na tuomba kupewa taarifa kwa sehemu yoyote ambapo kutatokea tatizo kama
hili na tutachukua hatua mara moja kuokoa fedha zilizotakiwa kwenda kusaidia
watu husika” Alisema Mhe Angella Kairuki.
Aidha Mhe. Angella Kairuki ameongeza kuwa
kuna taarifa zinazoenezwa kuwa fedha za mpango wa TASAF Awamu ya Tatu ni fedha
za freemasons, taarifa hizo sio za kweli kwani fedha hizi zizantolewa na
Serikali ili kusaidia Kaya maskini ili ziweze kujikwamua kiuchumi kwa kuweza kupata Elimu Malazi na chakula bora.
TASAF ni mpango wa
kunusuru Kaya maskini na imekuwa katika awamu tatu mpaka hadi sasa kwa ajili ya
kuwezesha Kaya maskini kujikwamua kiuchumi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni