 |
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi
mara baada ya kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo kabla ya kuelekea
kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo walemavu wa
ngozi cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
|

 |
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose
Nyamubi akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa
Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mshauri wa masuala ya haki za
binadamu kutoka ofisi kwake, Bi. Chitralekha Massey ( wa pili kulia kwake)
pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN)
Tanzania Hoyce Temu (wa pili kushoto). Wengine katika picha ni Afisa Elimu
Sayansikimu, Beatrice Mbonea (wa kwa kulia), Afisa Elimu Msingi wa manispaa ya
Shinyanga, Bi. Pudensiana Magnus (katikati kulia), Mkurugenzi wa manispaa ya
Shinyanga, Festo Kang'ombe pamoja na Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bw.
Shadrack Kengese.
|
 |
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE
SAME SUN, Vicky Ntetema alijumuika kwenye mazungumzo hayo. Pichani akifafanua
jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
(hayupo pichani) kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye
ulemavu wa ngozi nchini.
|
 |
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi
katika picha ya pamoja na ugeni kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa Tanzania na
Shirika la UNDER THE SAME SUN.
|
 |
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi
akiwasalimia watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo cha
Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga kabla ya
kumtambulisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
(hayupo pichani).
|
 |
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez (kulia) akizungumza na watoto wenye ulemavu wakiwemo wa ngozi (hawapo
pichani) wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani
Shinyanga alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho. Katikati ni Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu na
kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi.
|
 |
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akishiriki kwenye zoezi la kugawa zawadi kwa
watoto hao.
|
 |
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez akitoa zawadi ya maziwa kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa
kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
|
 |
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez na Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya
Mratibu huyo, Bi. Chitralekha Massey wakiendelea na zoezi la kugawa zawadi
kwa watoto hao.
|
 |
Pichani ni jiko la kituo cha kulelea watoto wenye
ulemavu wakiwemo wa ngozi cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
|
 |
Wapishi wakiendelea na shughuli zao kuwapikia
watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.
|
 |
Mwalimu Mkuu wa shule ya watoto wenye maalum ya
Buhangija Jumuishi, Peter Ajali akitoa maelezo ndani ya moja ya mabweni kituoni
hapo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
(kulia) na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE
SAME SUN, Vicky Ntetema.
|
 |
Mwalimu Mkuu wa shule ya watoto wenye maalum ya
Buhangija Jumuishi, Peter Ajali akimwonyesha baadhi ya sehemu ambazo
hazisakafiwa ndani ya mabweni kituoni hapo Mratibu Mkazi wa mashirika
ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
|
 |
Baadhi ya matandiko wanayotumia watoto hao wenye
mahitaji maalum kulali kwenye sakafu ambayo haijasakafiwa na pia kutokana na
uhaba wa mabweni inawalazimu kubanana na kulala bila uhuru.
|
 |
Bweni lililojengwa na Miss Tanzania 2012, Brigitte
Alfred linalohudumia watoto 48 ambalo linahitaji kumaliziwa ili watoto hao nao
waweze kulala mahali pazuri.
|
 |
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez akicheza mpira ambao ni moja ya zawadi alizozitoa kwa watoto wenye
ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo
mkoani Shinyanga alipofanya ziara ya kukitembelea kituo hicho kinachokabiliwa
na changamoto mbalimbali na kuwaahidi kuwasaidia huku akiwashirkisha na wadau
wengine wa maendeleo. Kushoto mwenye kofia ni Khassan Khamis na kulia ni
Emmanuel Deus.
|
 |
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez akisoma ujumbe unaosema "DREAM BIG" kwenye T-shirt ya mtoto
Agnes Kabika mwenye ulemavu wa ngozi anayelelewa kwenye kituo cha Buhangija
Jumuishi alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho
|
 |
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez akiwa amembeba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Ghoke Maliwa anayelelewa
kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga alipofanya ziara
ya kukitembelea kituo hicho juzi mkoani humo.
|
 |
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiagana na
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi mara baada ya kuhitimisha
ziara yake kwenye kituo hicho.
|
 |
Mratibu Mkazi huyo Bw. Alvaro Rodriguez
akiwasaidia watoto hao kufungua biskuti alizowapekea kama zawadi alipotembelea
kwenye kituo hicho.
|
 |
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez na Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya
Mratibu huyo, Bi. Chitralekha Massey wakiendelea na zoezi la kugawa zawadi
kwa watoto hao.
|
 |
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME
SUN, Vicky Ntetema akieleza jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja
wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) alipokuwa akikagua mazingira ya kituo hicho na
kuona ni jinsi atawasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili kituo
hicho.
|
 |
Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi
ya Mratibu huyo, Bi. Chitralekha Massey akibadilishana mawazo na binti
anayefanya shughuli za kujitolea Claire Grubbs kutoka nchini Marekani
aliyepiga kambi kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani
Shinyanga | | |
Picha kwa hisani ya MO Blog
Kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2010 kwa ajili ya watoto walemavu
wasiosikia na wasiiona kwa sasa kinapokea watoto wenye alibnizim ambao
wanaokabiliwa na ujahiri dhidi ya maisha yao.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa
wilaya kituo hicho ambacho serikali hutenga bajeti kwa ajili ya wanafunzi 50
wasiosikia na kuona, sasa kina watoto wenye albinism 247 ambao hawako katika
bajeti na wanaishi kutokana na misaada ya watu mbalimbali.
Alisema kwamba watoto wenye
albinism wanahitaji huduma za tiba za karibu zaidi kutokana na mazingira
yanawazunguka na dirisha pekee katika hospitali ya mkoa halitoshi kwani wakati
mwingine wanalazimika kukaa kwenye foleni kama wagonjwa wengine na hili
halipendezi.
Aidha alisema kituo hicho
cha Buhangija kwa sasa ni kidogo kuzingatia na uwingi wa wanaohitaji msaada na
hivyo serikali inatafuta eneo jingine kwa ajili ya kujenga kituo.
Kufurika kwa watoto hao
wenye ulemavu kunatokana na tishio la maisha yao hasa ukanda wa Ziwa ambapo
familia zao zimewakimbiza kituoni hapo kwa ajili ya usalama wao.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya
amesema kwamba kituo hicho hakina bajeti na kutaka wasamaria wema kuendelea
kuchangia ili watoto hao waendeshe maisha ya kawaida.
Naye Mratibu wa Mashirika
ya Umoja Mataifa yaliyopo nchini, Alvaro Rodrigues amesema kwamba Umoja wa
Mataifa utaendelea kusaidia kituo hicho na kuwataka wanaotunzwa hapo kutoacha
kuishi kama watoto kwani ndio tunu waliyonayo kwa sasa.
Aliongeza kwamba
anauchukua wimbo waliouimba ambao unazungumzia machungu ya maisha yao na kwenda
kuwaeleza watu wengine ili nao washiriki katika kubadilisha hali ya kuogofisha
na kuleta usalama.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE
SAME SUN, Vicky Ntetema alijumuika kwenye mazungumzo hayo. Pichani akifafanua
jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
(hayupo pichani) kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye
ulemavu wa ngozi nchini.
Alisema wao (UN) wamefika
katika kituo hicho kuona watoto wanavyoishi na watafanya nini kuwasaidia.
Aliwataka Watanzania
kuhakikisha wanakomesha machungu ya albino hao na kuishi nao kama watu wengine
wa kawaida.
Aidha Mratibu huyo alipata
nafasi ya kuzungumza na Binti wa miaka 19 Masabu masuka ambaye amejifungua
mwaka jana kituoni hapo bila msaada wa wauguzi baada ya kulazimika kuondoka
kwao akiwa mjamzito kukwepa mauaji dhidi ya albino yaliyofanyika Mei mwaka jana
wilayani Bariadi.
Binti huyo alifika kituoni
hapo na kaka zake watatu ambao wote ni maalbino kama yeye.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni