Jumatano, 8 Oktoba 2014

NMB yatoa msaada kwa ajili ya Wikiya Vijana na Kilele cha Mbio za Mwenge mkoani Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akipokea msaada wa T-Shirt na Kofia kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mihayo mkoani Tabora Bw. Festo Mashayo aliyekadidhi msaada huo kwa niaba ya Makao Makuu leo Mkoani Tabora. NMB wamekabidhi msaada wa T-Shirt na kofia 100 zenye thamani ya shilingi milioni 25 kwa ajili ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kilele cha Mbio za Mwenge ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani hapa.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, Meneja Uhusiano wa NMB Kanda ya Magharibi Bw. Madaha Peter na mwisho kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bibi. Kudra Mwinyimvua.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bibi. Kudra Mwinyimvua (kushoto) akipeana mkono na  Meneja wa NMB Tawi la Mihayo mkoani Tabora Bw. Festo Mashayo aliyekadidhi baada ya kupokea msaada wa T-Shirt na leo mkoani Tabora. NMB wamekabidhi msaada wa T-Shirt na kofia 100 zenye thamani ya shilingi milioni 25 kwa ajili ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kilele cha Mbio za Mwenge ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani hapa. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, Meneja Uhusiano wa NMB Kanda ya Magharibi Bw. Madaha Peter
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (Watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Tabaro na wawakilishi wa Benki ya NMB wakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano wa msaada wa T-Shirt na kofia. Kutoka kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Mihayo Bw. Festo Mashayo,Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bibi Fatma Mwassa,Meneja Uhusiano wa NMB Kanda ya Magharibi Madaha Peter, Katibu Tawala wa mkoa wa Tabora Bibi. Kudra Mwinyimvua, na Afisa Mikopo Tawi la Mihayo Stevene Mguruka.


Picha na Frank Shija

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Kumbukumbu la Blogu