Taarifa mbali mbali za utekelezaji wa
Shughuli za Chuo kwa muda wa Mwaka Julai
2013 – Juni 2014 ziliwasilishwa kwa Bodi ya Wadhamini.
Baadhi ya mafunzo yaliyofanywa na Chuo
kupitia Idara ya Utafiti, Ushauri na Mafunzo ya Muda Mfupi kwa kipindi cha
mwaka 2013/2014 ni yafuatayo:-
a) Mafunzo
ya kuwajengea uwezo Watunza kumbukumbu, Wahudumu, Wasimamizi wa Ofisi na
Makatibu Mhutasi wa halmashauri na taasisi zingine za Serikali yalifanyika hapa
Chuoni.
b) Mafunzo
kuhusu Sheria Mpya ya Manunuzi ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013, kwa
Wakuu wa Idara na waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.
c) Mafunzo
ya Uongozi na Utawala Bora kwa Wakuu wa Idara na waheshimiwa madiwani wa Halmashauri
ya Wilaya ya Tarime.
d) Mafunzo
ya stadi za Menejimenti na Uongozi kwa Halmashauri za Wilaya za Kibondo na
Kasulu.
e) Tathmini
ya Mahitaji ya Mafunzo kwa watumishi wa Halmashauri za Wilaya za Mkuranga,
Kigoma, Kasulu, Kibondo na Manispaa ya Kigoma, Kazi ya Ushauri (Consultancy)
chini ya Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (BTC)
f) Mafunzo
ya Utunzaji kumbukumbu na Usimamizi wa Ofisi kwa Watumishi wa Wilaya ya Rombo.
g) Mafunzo
ya Uwajibikaji wa Kijamii (Social Accountability) kwa Watumishi wa Mamlaka za
Serikali za Mitaa, Asasi za Kiraia na Mashirika ya dini kutoka Wilaya za
Karagwe, Ukerewe na Magu.
h)
Kuhusu uanzishaji wa Kozi za
Shahada (Bachelor Degree), Bodi ya Wadhamini kupitia kamati yake ya Taaluma
iliiagiza Menejimenti kuandaa andiko la hoja ya msingi kuhusu pendekezo hili na
uwezekano wa kutoa mafunzo ya kujenga weledi na stadi za kazi kwa Watumishi wa
Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia kozi za Shahada.
Aidha, miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na taarifa ya wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na Chuo cha Serikali za Mitaa kwa mwaka wa masomo
2014/2015. katika mwaka wa masomo 2014/2015 jumla ya wanafunzi wapya 1803
wamechaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali zitolewazo na Chuo cha Serikali za
Mitaa. Idadi hii inajumuisha wanafunzi waliochaguliwa moja kwa moja na wale
waliochaguliwa kupitia kozi ya “Pre-entry).
JEDWALI LIFUATALO LINAONESHA IDADI YA
WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA
Na.
|
KOZI
|
ME
|
KE
|
JUMLA
|
1.
|
Astashahada
ya Utawala katika Serikali za Mitaa (BTCLA)
|
165
|
170
|
335
|
2.
|
Astashahada ya Uhasibu na Fedha katika Serikali za
Mitaa (CLF)
|
36
|
19
|
55
|
3.
|
Astashahada
ya Maendeleo ya Jamii (BTCCD)
|
69
|
152
|
221
|
4.
|
Astashahada
ya Menejimenti ya Rasilimali Watu (BTCHRM)
|
46
|
78
|
124
|
5.
|
Stashahada
ya Utawala katika Serikali za Mitaa (DLA)
|
76
|
124
|
200
|
6.
|
Stashahada ya Uhasibu na Fedha katika Serikali za
Mitaa (DLF)
|
45
|
43
|
88
|
7.
|
Stashahada
ya Maendeleo ya Jamii (DCD)
|
79
|
150
|
229
|
8.
|
Stashahada
ya Menejimenti ya Rasilimali Watu (DHRM)
|
44
|
61
|
105
|
9.
|
Wanafunzi wa
“Pre-entry course”
|
152
|
294
|
446
|
|
JUMLA
|
712
|
1091
|
1803
|
Katika
mwaka wa fedha 2013/2014, Chuo kilipanga na kutekeleza miradi ya maendeleo kama
ifuatavyo:-
1) Ulipaji
wa Fidia wa Eneo jipya (ekari 637)
Hadi
mwisho wa Robo ya Nne ya mwaka wa fedha 2013/2014, Chuo kilikuwa kimepokea
jumla ya Sh.200,000,000 kwa ajili ya
kulipa fidia kwa wananchi ambao walikuwa katika mpango wa kulipwa. Vile vile, Chuo kilipokea Sh.350,000,000 kupitia ruzuku ya matumizi mengineyo kwa ajili ya
kulipa fidia kwa wananchi waliokuwa wamebaki kulipwa fidia katika bajeti ya
mwaka wa fedha 2012/2013. Kwa mantiki hiyo, Chuo sasa kimelipa fidia ya eneo lote
jipya lenye ukubwa wa ekari 637.
2) Ujenzi
wa Kituo cha Afya (Awamu ya Kwanza)
Ujenzi
wa kituo cha Afya ( Awamu ya kwanza) ambao ulianza tarehe 09/09/2013 kwa
kuhusisha majengo matatu ambayo ni Maabara (Laboratory Block), Matibabu
(Treatment Block) na Watabibu (Consultation Block) umekamilika kwa 95%
Chuo cha Serikali za Mitaa ni miongoni mwa Taasisi zilizoko
chini ya OWM-TAMISEMI na kilianzishwa kwa mujibu wa Sheria Na. 26 ya mwaka 1994
(Sura ya 396 toleo lililorejewa mwaka 2002). Lengo kuu la kuanzishwa kwake ni
kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kutoa huduma bora
zitakazowajengea wananchi uwezo wa kuimarisha utawala bora, kuondokana na
umaskini na kuboresha maisha yao. Pia Chuo ni Taasisi Kiongozi ya Mafunzo (Lead
Training Institution) kikiwa na majuku ya kuratibu mafuinzo yote yanayotolewa
kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa, Kudhibiti ubora wa Mafunzo yanayotolewa
kwa Mamlaka za Serikali za Mitaala na kuandaa Mitaala mbali mbali yakufundishia.
Majukumu ya Chuo yamegawanyika katika sehemu kuu
tatu:-
Kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu juu ya taaluma,
ujuzi, stadi na mbinu za uendeshaji wa Serikali za Mitaa kwa Viongozi na
Watumishi walio katika ngazi mbalimbali za Serikali za Mitaa;
Kutoa mafunzo juu ya mabadiliko yanayohusu Serikali za
Mitaa kulingana na Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa na;
Kufanya utafiti na kutoa ushauri kwa Serikali Kuu,
Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mashirika na watu binafsi juu ya masuala yote
yanayohusu Serikali za Mitaa.
BODI YA WADHAMINI ILIPISHA WATUMISHI WANAOENDA
MASOMONI
MWAKA WA FEDHA 2014/2014 KAMA IFUATAVYO
S/N
|
JINA
|
KOZI ANAYOENDA KUSOMA
|
UFADHILI
|
IDARA ANAYOTOKA
|
1.
|
Natangalia
Kalimangasi
|
PhD
|
Chuo
|
Taaluma
|
2.
|
Jonas
Kapwani
|
Masters
|
Chuo
|
Taaluma
|
3.
|
Isdory
Nyoni
|
Masters
|
Chuo
|
Taaluma
|
4.
|
Cyprian
Mbugano
|
Masters
|
Chuo
|
Utawala
|
5.
|
Grace
Majura
|
Diploma
|
Chuo
|
Utawala
|
6.
|
Veronica
Nahodha
|
Bachelor
|
Chuo
|
Utawala
|
Imetolewa na:
Public Relations Officer
Chuo Cha Serikali za Mitaa, Hombolo Dodoma
12.09.2014
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni