Frank
Mvungi-Maelezo
Mamlaka
ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekamilisha mradi wa kuboresha kituo cha
kupokea na kutuma mawasiliano ya radio zinazotumika katika usafiri wa anga kilichoko
Mnyuzi mkoani Tanga.
Mradi
huo uliojengwa na kampuni ya JOTRON ya
NORWAY umegharimu Serikali zaidi ya shilingi milioni 200 na ulikabidhiwa rasmi
kwa TCAA mapema mwezi Agosti mwaka huu.
Hayo
yamesemwa na Afisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi.
Bestina Magutu wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam.
Magutu
alisema kuwa kukamilika kwa kituo hicho
kumeongeza ufanisi wa utoaji huduma za uongozaji ndege na kuimarisha zaidi
usalama wa safari za anga hapa nchini.
Akifafanua
zaidi Magutu amesema hali hiyo itachangia kuongezeka kwa mapato ya Mamlaka hiyo
yanayotokana na tozo la huduma za uongozaji ndege.
Akizungumzia
mikakati ya Mamlaka hiyo Magutu amesema inaendelea kuwekeza katika miundo mbinu
ya kuongozea ndege hivyo kwenda sanjari na mabadiliko ya teknolojia pamoja na
kumudu ukuaji wa Sekta ya usafiri wa anga hapa nchini.
Katika
hatua nyingine Mamlaka hiyo imesema kuwa wanafunzi watano waliopewa
ufadhili wa kusomea urubani nchini
Afrika ya Kusini wameendelea kupata ufaulu wa juu na kushika nafasi ya kwanza
hadi ya tano katika darasa la watu 14 katika shule ya urubani nchini Afrika ya
Kusini.
Takwimu
za mwaka 2013 zinaonyesha ongezeko la miruko ya ndege ( flight movements)
kutoka 222,430 mwaka 2012 hadi kufikia miruko 230,458 sawa na ongezeko la
asilimia 3.6 kadhalika katika kipindi hicho idadi ya abiria imeongezeka kutoka
4,056,925 hadi kufikia 4,626,016 sawa na ongezeko la asilimia 14.Idadi ya
abiria inatarajiwa kufika zaidi ya milioni 5 kufikia mwishoni mwa mwaka 2014.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni